MWANAMUME mmoja mwenye umri wa miaka 30 amejikuta kwenye njia panda baada ya mke wa marehemu babake kudhihirisha hisia za mapenzi kwake na hata kumwandikia barua akimuarifu hilo.

Kijana huyo alieleza mafadhaiko yake kupitia kwa mtumizi mmoja wa mitandao ya kijamii anayetoa nafasi kwa watu kueleza masaibu yao kwa ahadi ya kutotambuliwa kwa majina yao na picha.

Alionekana kuzama katika bahari ya luja na kusimulia kwamba anamheshimu sana mama mdogo lakini sasa hajui itakuwaje maana mama ameshamtaarifu utayarifu wake wa kuwa katika mapenzi naye.

Alisema kwamba babake alifariki miaka 8 iliyopita, na miaka 5 baadae, mama wa kambo akaanza kumpa ishara na dalili zote za kumtaka kimapenzi licha ya kuwa ni mama mwenye umri wa miaka 36.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alisimulia hivi: “Siku njema, Mkuu. Nilimpoteza baba yangu miaka 8 iliyopita. Alikuwa na wake wawili, mama yangu akiwa mkubwa. Ninafanya kazi katika sekta ya madini na kupata kiasi kinachostahili. Nina umri wa miaka 30, wakati mke mdogo wa baba yangu ana miaka 36 na watoto wawili (alipoteza mmoja kwa sababu ya ugonjwa). Zaidi ya miaka mitatu iliyopita, aliniambia kwa kawaida kuwa alikuwa akikuza hisia kwa ajili yangu na alihisi nilipaswa kujua. Sikulichukulia kwa uzito wakati huo.”



Akifikiria ni mzaha, kijana huyo alipata mama wa kambo amemtumia zawadi maridadi siku yake ya kuzaliwa mapema mwaka huu.

Japo alikiri kwamba si mara ya kwanza kwa mama wa kambo kumtumia zawadi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, alisema safari hii zawadi iliambatanishwa na barua ya kumkumbusha kuhusu hisia zake za mapenzi kwake.

Jambo hilo lilimpiga dafrau ghafla na kujipata katika njia panda huku akiomba ushauri wa jinsi ya kutatua suala hilo baina yake na mke mdogo wa marehemu babake.

"Ili kufupisha kila kitu, siku yangu ya kuzaliwa mnamo Machi, alinitumia zawadi, kama kawaida yake kila mwaka, lakini wakati huu ilikuja na barua. Katika barua hiyo, aliandika kwamba anakufa moyoni kwa sababu hawezi tena kudhibiti hisia zake kwangu.”



Ufichuzi wa kushtua wa mwanamume huyo ulienea haraka, huku watu wengi waliohusika walifurika sehemu ya maoni ili kutoa ushauri.

Baadhi walimtaka kupotezea uwezekano wa kutokea kwa kitu chochote baina yake na mke wa babake wakisema kuwa hafai hata kuendekeza hisia za mapenzi kwa mtu aliyeonana kimwili na babake mzazi.

Walimshauri kutorudi nyumbani kabisa na ikiwezekana kukata mawasiliano na mama wa kambo.

Hata hivyo, watoro wengine wa maadili walimtaka kudakia fursa hiyo, wakisema kwamba pengo la umri kati yao ni miaka 6 tu ambalo kwao si pengo kubwa.

Je, wewe una ungepata nafasi ya kuketi chini na kijana huyu, ungemshauri vipi?