Kijana aliyevuma kwa kuutetea kwa sauti kubwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) wakati wa maandamano ya kupinga serikali mapema mwaka huu hatimaye amepata nafasi ya kupanda ndege.

Mchekeshaji Eric Omondi, ambaye mnamo Septemba, alisaidia kuchangisha pesa za masomo yake ya chuo kikuu ya Henry, amefichua kuwa kijana huyo alitua katika uwanja wa JKIA kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu asubuhi.

Katika taarifa yake kwenye Instagram, Eric alitambua juhudi kubwa za Henry kuokoa uwanja wa ndege wa JKIA dhidi ya madai ya kuuzwa, na akamshukuru kwa hilo.

“Ndugu yetu leo ​​amepanda ndege na kutua JKIA kwa mara ya kwanza kabisa. Tunasherehekea na kumthamini,” Eric Omondi alisema.

Mchekeshaji huyo pia alithibitisha kuwa Henry tayari anaendelea na chuo na anasomea ufundi mekanika.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Pia aliwaomba watu wenye mapenzi mema kuendelea kusaidia elimu yake kwa kutuma fedha kwa mama yake.

“Tulimsajili kwenye TVET. Anataka kuwa fundi. Namba yake ni 0790 166983 Jina itasema Mourine Ochieng(The Mother). Hebu tumthamini. Anastahili,” alisema.

Henry alipata umaarufu mkubwa mwezi wa Julai baada ya video yake akipinga madai ya kuuzwa kwa JKIA kuvuma kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo, kijana huyo alidai kuwa rais Ruto alikuwa akiuza uwanja wa ndege kwa mtu kutoka India.

“Ameuza airport, ameuzia muhindi. Sijui huyo muhindi,” alisikika Henry akisema.

Eric Omondi baadaye aliweza kumtafuta na kumsajili kwa elimu ya chuo kikuu katika Tvet Ndere Polytechnic.