Chelsea wameungana na Arsenal katika mbio za kumnasa Alexander Isak - lakini Newcastle United itadai angalau pauni milioni 115 kwa mshambuliaji wao wa Uswidi mwenye umri wa miaka 25. (TeamTalks),

Aston Villa, AC Milan na Juventus zitamenyana na Arsenal kumnunua fowadi wa Real Madrid Arda Guler, 19, huku klabu hiyo ya Uhispania sasa ikifahamika kuwa iko tayari kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki kuondoka kwa mkopo. (Caughtoffside)

Klabu ya Hamburg ya Ujerumani inafikiria kumteua kocha wa muda wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy kama meneja wao mpya baada ya kuachana na Steffen Baumgart. (Sky Sports Germany),

Mkufunzi wa Fenerbahce Jose Mourinho amepuuzilia mbali uvumi kuhusu klabu hiyo ya Uturuki kutaka kumnunua mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 39 Cristiano Ronaldo. (Goal)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Cristiano Ronaldo
Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kiungo wa kati wa Lille na England Angel Gomes, 24, anatazamiwa kurejea Manchester United baada ya meneja mpya Ruben Amorim kuipa klabu hiyo ruhusa kumnunua tena. (Caughtoffside), nje

Nottingham Forest wapo kwenye mazungumzo na beki wa pembeni Ola Aina kuhusu mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 28 unamalizika msimu wa joto, kumaanisha kuwa atakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu za ng'ambo kuanzia Januari. (Athletic – Subscription Required)

Meneja wa Crystal Palace Oliver Glasner ataungwa mkono pakubwa katika soko la usajili la Januari huku raia huyo wa Austria akijizatiti kuimarisha kikosi chake kilicho hatarini kushuka daraja. (Football Insider)

Real Sociedad wanahisi kutokuwa na uwezo wa kumzuia mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Martin Zubimendi, 25, kuondoka katika klabu hiyo, huku Arsenal na Liverpool zote zikiwa na hamu ya kumsajili kiungo huyo ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya euro 60m (£49.9m). (Todofichajes – In Spanish).

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Martin Zubimendi

Wayne Rooney anapanga kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Muingereza Jayden Danns, 18, ili kuimarisha safu yake ya mashambulizi Plymouth. (Sun)

Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe na mkurugenzi wa michezo Paul Mitchell wamefanya mazungumzo ya mapema na wamiliki wa klabu hiyo kutoka Saudi Arabia kujadili mipango yao ya soko la uhamisho la Januari wakati kipa wa Slovakia Martin Dubravka, 35, anaweza kuondoka. (Chronicle Times)

Manchester City wanavutiwa na beki wa kati wa Bournemouth Illia Zabarnyi na The Cherries wanaweza kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine mwenye umri wa miaka 22 katika msimu wa joto ili kutafuta fedha. (Football Insider)