Odinga

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga mnamo Alhamisi alipata fursa ya kukutana na rais wa Togo Faure Essozimma Gnassingbe huku akiendelea kuomba uungwaji mkono kwa kiti cha uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

 

Katika taarifa yake Jumamosi asubuhi, mwanasiasa huyo aliyegombea urais wa Kenya kwa mara tano alibainisha kuwa alishiriki mashauri yenye mafanikio na rais Gnassingbe.

 

Raila alifichua kuwa pamoja na masuala mengine, walijadili matatizo yanayokabili bara la Afrika na suluhu zinazowezekana. Pia alipata fursa ya kuomba uungwaji mkono wa Togo kabla ya uchaguzi wa AUC mwaka ujao.

‘Nilikuwa na mashauri yenye manufaa na Rais Faure Gnassingbé wa Togo, kuhusu fursa, changamoto, na masuluhisho yanayoweza kukabili bara la Afrika,” Raila alisema kupitia akaunti yake ya X.

"Ushirikiano wangu na viongozi kote barani ni sehemu ya programu yangu ya kufikia watu ili kutafuta uungwaji mkono kwa ajili ya zabuni yangu ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika," aliongeza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Rais Gnassingbe wa Togo alithibitisha kukutana na Raila na kufichua kuwa walikuwa na mijadala kuhusu hali ya kisiasa na usalama barani Afrika. 

‘Rais wa Jamhuri, @FEGnassingbe mnamo Alhamisi, Novemba 21, 2024, amekutana na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, @RailaOdinga.Miongoni mwa mada za ni, hali ya kisiasa na kiusalama barani Afrika pamoja na changamoto za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. barani,” ikulu ya Togo ilisema.

Uchaguzi wa Tume ya Umoja wa Afrika utafanyika Februari 2025 na Raila Odinga amekuwa akisafiri kote barani Afrika akijipigia debe na kuomba kuungwa mkono.

 

Mnamo Novemba 8, Raila Odinga alizindua rasmi ugombeaji wake wa nafasi ya juu katika Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, akijitambulisha kama "mfuko kamili" unaohitajika kukabiliana na migogoro na uchumi wa Afrika.