KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi Novemba 23.  

 

Katika taarifa ya Ijumaa jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

 

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja unusu  jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Kisumu na Siaya.

Katika kaunti ya Kisumu, eneo la soko ya Riat litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa sita adhuhuri.

Maeneo ya Kisumu Poly na Manyatta yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika kaunti ya Siaya, maeneo ya Tingwangi, Anduro na Malanga yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Pap Kadero na Madiany pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.