Muigizaji mashuhuri wa Kenya Catherine Kamau almaarufu Kate Actress ni mama mwenye furaha kufuatia hatua kubwa katika maisha ya mwanawe.
Leon Kamau, mtoto wa kwanza wa Kate, alifanya mtihani wa KCSE 2024 na kumaliza Alhamisi, na muigizaji huyo mahiri hakuweza kuficha furaha yake.
Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kate alimshukuru Mungu kwa mafanikio makubwa ya mwanawe.
“Mungu mpendwa, asante. Sio mara moja tuliita jina lako, mara kwa mara ulijitokeza kwa ajili ya mtoto wangu. Tumerudi kusema ASANTE MUNGU,” Kate Actress aliandika.
Muigizaji huyo mwenye kipawa pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru familia yake, marafiki, walimu na aliyekuwa mume wake Phil Karanja kwa majukumu yao katika mafanikio ya Leon.
“Kwa familia yangu, marafiki zangu wapendwa, Baba Njeri @Phil_director, walimu wake, asanteni sana. Mungu awabariki nyote,” alisema.
Aliongeza, "Hey Lee, tumefanya haya baby."
Mwanawe Kate, Leon Kamau, alitimiza umri wa miaka 18, mwezi Julai, hatua inayomruhusu kutambuliwa rasmi kama mtu mzima nchini Kenya.
Kate alitumia fursa hiyo kusherehekea mwanawe kwa ujumbe maalum, akielezea kujali kwake kwa mbegu ya tumbo lake haswa katika wakati ambapo maisha ya vijana wengi wa Kenya yanachukuliwa kuwa hatarini.
"Nina hisia sana leo ?, Kheri ya siku ya kuzaliwa ya 18 mtoto wangu mkubwa . Pamoja na yote yanayoendelea kutuzunguka,? akina mama kupoteza watoto wao wa kiume wasio na hatia kwa ukatili wa polisi & dhulma zingine anazofanyiwa mtoto wa kiume mweusi katika jamii ya sasa, nataka nikusogezee karibu zaidi leo, kwa kumshukuru Mungu sana kwa kupata. wewe kwa Umri huu mkubwa. Tulifanya mtoto wangu. Kheri ya siku ya kuzaliwa roho yangu,” Kate Actress alimwandikia mwanawe.
Muigizaji huyo mashuhuri aliambatanisha ujumbe wake na picha
ya kumbukumbu yake na Leon, na sala maalum sana kwa mvulana wa miaka 18.
Leon alizaliwa miaka mingi iliyopita wakati Kate alikuwa anaendeleza masomo yake ya chuo kikuu katika nchi jirani ya Uganda.
Katika mahojiano ya miaka michache iliyopita, muigizaji huyo mahiri alifichua kuwa alipachikwa ujauzito wa kifungua mimba hicho chake miezi mitatu tu baada ya kujiunga na chuo kikuu cha Kampala.
Kate alikiri kuwa aliponda raha kweli kuanzia siku za kwanza alipojiunga na chuo kikuu na alishtuka sana wakati daktari alipomvunjia habari kuhusu ujauzito wake.
"Ilikuwa kama uhuru. Ningeweza kuenda nje. Tulikuwa karibu na Kabaragala, hepi kila wakati.. tulidunda. Hata sikupumua, miezi mitatu nikabeba ujauzito. Sikuelewa jinsi ilikuwa mshtuko kwangu, ilikuja haraka. Hata daktari aliponiambia sikuamini. Nilikuwa msichana mdogo na mtu hangejua. Sikufahamu kuhusu kutumia mbinu za kuzuia ujauzito. Niliendea dawa za 'Morning after' baada ya wiki tatu " Cate alisimulia katika mahojiano na Churchill.
Muigizaji huyo alidai kuwa jamaa aliyempachika ujauzito alimsaidia siku za kwanza lakini baada ya kuona jinsi mambo yalivyoendelea kuwa mazito akamuacha.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!