Timu zote 24 za Afrika ambazo zitashiriki katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 (Afcon 2025) zimethibitishwa rasmi.

Haya yanajiri baada ya kukamilika kwa mechi za kufuzu Afcon 2025 mnamo siku ya Jumanne usiku.

Mataifa matatu ya mwisho kuhifadhi nafasi zao katika mashindano ya mwaka ujao yalikuwa ni Tanzania, Botswana, na Msumbiji.

Timu 21tayari zilikuwa zimefuzu kwa dimba hilo kabla ya mechi za mwisho za Jumanne.

Tazama orodha kamili ya timu zilizohitimu:

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

o Morocco.

o Burkina Faso.

o Cameroon.

o Algeria.

o DR Congo.

o Senegal.

o Misri.

o Angola.

o Gabon.

o Uganda.

o Afrika Kusini.

o Equitorial Guinea.

o Cote d'Ivoire.

o Nigeria.

o Jamhuri ya Benin.

o Comoros

o Sudan.

o Zimbabwe.

o Mali.

o Zambia.

o Tunisia.

o Tanzania.

o Botswana.

o Msumbiji.


Mashindano ya Afcon 2025 yatafanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026.