MREMBO mmoja mwenye umri wa makamo amezua mjadala na vichekesho kwenye mtandao wa kijamii baada ya kusimulia jinsi alitumia ujanja wake wa kuzaliwa kukwepa mfarakano na mke halali wa mpenzi wake.

Mrembo huyo ambaye alikiri kuwa mpango wa kando kwa mwanamume huyo, alisimulia kwamba walikuwa ndani ya gari la mwanamume huyo wakienda kujivinjari.

Ghafla, mke halali wa mwanamume wake alitokea na ikambidi kujiongeza na kutafuta njia ya kuponyoka garini ili kuepusha vita na mke halali.

Mrembo huyo alijitosa ndani ya buti la gari hilo na kuvumilia joto kali akiwa hana lolote la kufanya.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Nilienda kwenye date na mwanamume wa mwenyewe, mke wake karibu atufumanie, namshukuru Mungu aliokoa maisha yangu,” aliandika kwenye video hiyo huku akionyesha jinsi alivyojifinyilia ndani ya buti la gari hilo dogo.

Chapisho hilo lilizua maoni kinzani kutoka kwa watu, wengine wakimpongeza kwa kutumia akili na busara kujinasua.

Hata hivyo, wengine walimsuta kwa kumshukuru Mungu kumuokoa hali ya kuwa alikuwa anafanya jambo lisilofurahisha machoni pa Mungu, tena akiwa anajua.

Hata hivyo, wengine walimsuta wakidai kwamba alisimulia kisa kisichokuwa cha kweli kwa ajili ya kutafuta kiki mitandaoni.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

callmegrace??: "Nah Mungu akuokoe dada yangu ?."

Smith: "na wakati huo mke anataka kutumia gari ???."

she_is_luchy?: "nawaooo ooo natamani wanaume wote waliooa waogope kuwa na wake kama hawa."

Selena: "Ninyi watu mnastarehe vipi kuchapisha vitu hivi."