MJASIRIAMALI na msanii Esther Akoth maarufu kama Akothee amewasuta wale wanaokosoa mtindo wa maisha yake katika mitandao ya kijamii.

Akothee amewapa changamoto wakosoaji wake kuweka wazi mafanikio yao wakiwa na umri wa miaka 32, akisema kwamba yeye akiwa na umri huo mwaka 2013, alifanikisha kujijengea jumba la kifahari.

Akothee alijijengea jumba la kifahari nyumbani kwao katika kaunti ya Migori, moja kati ya miradi mingi ambayo anajivunia kuifanikisha bila mikopo wala madeni.

“Kabla hujaingizwa na maisha yangu pata uchungu na hasira. Ulikuwa wapi mwaka 2013 na una umri gani kwa sasa? Utakuwa wapi ndani ya miaka 10 kuanzia sasa, na je unafanya kazi kuelekea lengo hilo?”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Mnamo 2013 Nikiwa na umri wa miaka 32, tayari nilikuwa nimewazia jinsi mpango wangu wa kustaafu ungekuwa, na nilichukua hatua za makusudi kuufanya kuwa hai. Muundo unaouona ni nyumba yangu ya kustaafu huko Rongo, Kamagambo—ushuhuda wa shauku na ustadi wangu kama msanidi programu.”

“Mimi binafsi nilisimamia ujenzi wa mali zangu zote, nikiendeshwa na maono wazi ya kile nilichotaka kufikia. Kujenga nyumba hii ilikuwa safari ya kuridhisha sana, iliyokamilika bila deni kabisa. Na mikopo sifuri,” Akothee alisema.

Mama huyo wa watoto 5 alifichua kwamba kipindi anasimika msingi wa mradi huo wa kipekee, alikwepa suala lolote la mapenzi katika maisha yake, lakini licha ya kujikita katika kufuatilia na kusimamia ujenzi huo, aliweza pia kutenga muda wa kujivinjari kwa kutembea duniani kote, lakini pia kuwaelimisha wanawe, ndugu zake na hata baadhi ya watoto wa watu ambao alikuwa anasaidia kufadhili ndoto zao kimasomo.

“Licha ya mahitaji ya kifedha, nilisawazisha kujenga nyumba yangu, kusafiri ulimwengu, kusomesha watoto wangu ndugu zangu na watoto wa watu wengine bila kuathiri malengo yangu. Uchumba haukuwa kipaumbele; kwa kweli, niliepuka wanaume kabisa katika kipindi hiki, nikizingatia badala yake kuunda urithi na nafasi salama kwa watoto wangu,” alisema.

Baada ya kumaliza ujenzi wa jumba lake, Akothee alifichua kuwa aliwajengea pia wazazi wake kama njia moja ya kurudisha shukrani kwa malezi yao kwake.

“Mara nilipomaliza nyumba yangu, nilielekeza mawazo yangu katika kujenga nyumba kwa ajili ya mama yangu—ishara ya shukrani na upendo.”

“Kwa hivyo, unaponiona nikifurahia maisha na kurukaruka, kumbuka kwamba nilianza kwa kutanguliza kilicho muhimu sana,” alimaliza kwa ushauri.