
Mhadhiri wa chuo kimoja nchini Uganda ametoa onyo
kali kwa vijana waliopo chuoni dhidi ya kusikiliza na kutazama wimbo wa
Hozambee.
Katika video ambayo imekuwa ikipiga misele katika
mitandao ya kijamii, mhadhiri huyo ambaye alikuwa anatoa wosia kwa mamia ya
wanafunzi katika ukumbi mmoja aliwaambia kwamba wimbo wa Hozambee si wa
kusikilizwa.
Aliwafokea akisema kwamba yeyote anayetazama au
kusikiliza wimbo huo hawezi kuwa na fanaka maishani, akiutaja wimbo huo kuwa
mbaya.
“Mnajua
chenye mnafanya kwenye mtandao, mnatazama kuna wimbo Fulani wa kishetani nchini
Uganda, sidhani hata kama kuna mtu yeyote anayetazama wimbo huo atafanikiwa
maishani. Wimbo huo ni wa kijinga sana, ni Hozambee…”
mhadhiri huyo alisema huku akijaribu kuiga kuuimba.
Mhadhiri huyo alisema kwamba wakati wa ujana wake,
hawakuwa wanasikiliza nyimbo za aina hiyo bali walikuwa wamejikita sana katika
kusikiliza nyimbo za mapinduzi kutoka Afrika Kusini.
“Mnacheka
lakini achene niwaambie, wakati tunakua tulikuwa tunasikiliza nyimbo kutoka
Afrika Kusini kuhusu mapinduzi. Tulikua tukiwa wapiganaji. Sasa nyinyi
mnasikiliza Hozambee,” aliwasxuta vijana.
Aliendelea mbele akisema jinsi kizazi cha sasa barani
Afrika kimepotoka kutokana na ujio wa utandawazi, akisema kuwa hata watoto wa
chekechea kutoka nchini Uchina wanafanya mambo ya muhimu kuliko vijana wa vyuo
vikuu barani Afrika ambao muda wao mwingi unaishia kwenye mitandao ya kijamii.
“Achene
niwaambie, watoto wa chekechea nchini Uchina sasa hivi wanafunzwa jinsi ya
kutengeneza midoli, na nyinyi hapa mnaimba Hoozambee. Haya ni maajabu. Hivyo,
vifaa vtya kielektroniki mlivyo navyo vinaweza kuwaunganisha na watu wenye
akili au kwa watu wanaoimba Hoozambee,” alisema.
Msomi huyo alisema kwamba mambo yanayoendelezwa na
vijana katika jamii ya kisasa yanamfanya kujihisi mgonjwa na ndio maana
anapenda kuwa mbali na kila kitu.
Wimbo wa Hoozambe uliachiwa takribani miezi 5
iliyopita na msanii Mudra D Viral akimshirikisha D Star na mrembo Shifura
kwenye video kama vixen.
Wimbo huo mpaka sasa umetazamwa mara milioni 8.5
kwenye jukwaa la video la YouTube.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!