Mtoto aliyedhoofika alipatikana akicheza kando ya mwili wa mamake saa chache baada ya kufariki katika nyumba katika eneo la Karinde, Kikuyu, Kaunti ya Kiambu.
Mama huyo anaaminika kuuawa na babake mvulana huyo ambaye baadaye alifariki kwa kujitoa uhai.
Miili yote miwili iligunduliwa ndani ya nyumba hiyo mnamo Jumapili, Novemba 17 jioni muda mrefu baada ya tukio hilo kutokea. Nyumba ilikuwa imefungwa kwa ndani,
Polisi walisema wanachunguza mauaji na kujitoa uhai katika tukio hilo.
Mwili wa mwanamume huyo aliyetambulika kwa jina la Reuben Ndede ulipatikana ukining’inia juu ya nguzo ya paa.
Mwanamke hakutambuliwa mara moja. Haijulikani ni lini walikufa, polisi walisema.
Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema miili hiyo miwili ilikuwa imeanza kuoza ikiashiria kwamba wawili hao walikufa karibu siku moja au zaidi mapema.
Wenyeji waliwapigia simu polisi wakisema wanandoa hao walikuwa wamekufa katika nyumba yao.
Mwili wa mwanamke huyo ulikuwa umelala sakafuni ukiwa na majeraha yanayoonekana. Mtoto mwenye umri wa takriban mwaka mmoja na nusu alikuwa amelala karibu na mwili.
Wa mwanaume ulikuwa unaning'inia kwenye kamba chumbani.
Kamanda wa polisi wa Kiambu Michael Muchiri alisema chanzo cha kisa hicho bado hakijajulikana.
Mtoto alikimbizwa katika hospitali ya Mutuini ambako alilazwa akiwa katika hali nzuri, polisi walisema.
Walioshuhudia walisema mtoto huyo alionekana amedhoofika na alionekana kutokuwa na chakula kwa zaidi ya siku moja.
Miili ya wanandoa hao ilihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City ikisubiri uchunguzi wa maiti na uchunguzi mwingine.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!