Saa chache baada ya msanii Willy Paul kumuomba Bahati na familia yake msamaha kwa mifarakano ya awali iliyoishia mahakamani, Bahati amevunja kimya chake.

Akichukua kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bahati alichapisha picha ya zamani wakiwa pamoja na Willy Paul wakati wanahangaika kutoboa tundu kwenye Sanaa ya injili.

Alianza kwa kukubali msamaha wake na kumkumbusha jinsi walikuwa wanahangaika juu chini katika mtaa duni wa Mathare enzi za nyuma.

Alimalizia kwa kumtaja kama ‘kaka wa milele’ na kusema kwamba Mungu ni wa nafasi ya pili, huku akimshauri kuungana naye kuendeleza Sanaa badala ya kuendeleza bifu.

“Ndugu Yangu @willy.paul.msafi ,Msamaha Umekubaliwa ? Tumetoka mbali, Sote tumepambana na changamoto nyingi na umasikini mkubwa katika Vitongoji duni vya Mathare ili kuwa hivi tulivyo leo na tunapojitahidi kuinuka na kuwa wakuu katika njia tumefanya makosa mengi lakini cha muhimu ni kurudi nyuma na kurekebisha pale tunapofikiri tulikosea kwani Mungu wetu ni Mungu wa Upendo na nafasi ya Pili. Zaidi ya yote hakuna kosa kubwa kuliko udugu tunaoshiriki,” Bahati alisema.

Awali, Willy Paul alichapisha picha ya familia nzima ya Bahati, na kuandika ujumbe akijuta jinsi alijipata katika hali ya kukorofishana na Diana Marua.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alichukua fursa hiyo kuomba msamaha Diana na watoto kwa kile alichokitaja kuwa ni kuwaingiza katika zogo lake na Bahati.

“Nikikumbuka mambo niliyojionea na kaka yangu, ninatambua kwamba mara kwa mara nimevuka mipaka. Ninashikilia sana dhana ya familia, haswa watoto. Matendo yangu hayakukusudiwa kamwe kusababisha madhara, lakini ninaelewa kwamba yalionekana hivyo, na ninaomba msamaha kwa Diana na watoto Kwa Upendo wa Kutokuelewana,” Willy Paul aliandika.

Itakumbukwa Willy Paul na Diana mnamo 2021 walipapurana vikali kwenye mitandao ya kijamii wakishushiana shutuma mbaya ambazo zilitishia kusambaratisha kabisa maisha ya Sanaa ya kila mmoja wao.

Diana alirekodi video akihadithia baina ya vilio kile alichodai kuwa ni kudhulumiwa kingono na Willy Paul, jambo ambalo Pozee alielekea mahakamani akidai ni kuchafuliwa sifa.

Mahakama ilimuamuru Marua kufuta video ile mara moja huku kesi hiyo ikijikokota mahakamani hadi hivi majuzi ambapo Pozee alifichua kuwa madai dhidi yake yametupiliwa mbali.