Msanii na rapa Stevo Simple Boy amegeuza ukurasa wake wa Instagram kuwa kanisa ya kipekee na kuwapakulia neno mashabiki na wafuasi wake.

Msanii huyo ambaye aliibuka akiwa amevalia suti ya samawati na mkononi amejihami na Biblia, aliwahubiria mashabiki wake akisema kwamba angefurahi kila mmoja wao angemsikiliza na kupata wokovu.

Msanii huyo wa ‘Mihadarati’ aliwataka vijana kutafuta wokovu ili kujinafasi katika safari ya mbinguni, akiwataka pia kutoingia kwenye majaribu ya uzinzi haswa wakati huu wa kijibaridi kikali.

“Bwana Yesu asifiwe, watuwangu wa kanisa, mimi kama Askofu Stevo Simple Boy, nawaambia mpende Mungu sana, muache usherati, muache mihadarati, muache uzinzi na matendo maovu na mtabarikiwa, au sio,” Stevo alihubiri huku akimalizia, “okoka tuende mbinguni.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Msanii huyo amekuwa akitajwa kama mtu mwenye uwezi wa kufanya mambo ainati kutoka kwa kuimba, ucheshi na sasa hata kuhubiri.

Stevo Simple Boy anatarajia kusherehekea miaka 5 ya usanii wake, hafla ambayo itafanyika mapema mwezi ujao katika mgahawa mmoja mjini Kisii.

Msanii huyo aliingia kwa kishindo cha kipekee kwenye tasnia ya muziki mwaka 2019 ambapo kibao chake cha kwanza ‘Mihadarati’ kilipokelewa kwa shangwe na mbwembwe kutoka kwa mashabiki wake.

Tangu wakati huo, wengi wameshindwa kujizuia kwa ngoma zake ambazo zinakuwa na ujumbe wa kuchekesha haswa kwa chaguzi za maneno anayotumia yenye maana fiche.