
Mkali wa muziki wa Nigeria, Daniel Anidugbe,
almaarufu Kizz Daniel, amewashangaza mashabiki kwa habari za mapumziko ya hivi
karibuni ya muziki.
Mwimbaji huyo alifichua kuwa atapumzika kuachia
muziki mpya hadi 2026, baada ya kuzindua EP yake inayotarajiwa sana, Uncle K,
ambayo itashuka mnamo Novemba 29, 2024.
"Baada
ya haya, sitaachia chochote tena hadi 2026,"
alitangaza kwenye ukurasa wake wa X mnamo Ijumaa, na kuzua hisia kutoka kwa
mashabiki ambao walionyesha hisia zao tofauti kwa kufikiria kutokuwepo kwake
kwenye uwanja wa muziki.
Tangu wimbo wake wa Woju kuvuma mwaka wa 2016, Kizz
Daniel ameimarisha nafasi yake kama mmoja wa waimbaji maarufu wa Nigeria,
akijivunia albamu tano za studio na orodha ya kuvutia ya nyimbo bora zaidi za
chati.
Huku kukiwa na gumzo karibu na likizo yake, msanii
huyo alishiriki mkasa wa kibinafsi, akifichua kwamba mke wake alifiwa na mama
yake hivi majuzi kutokana na saratani ya matiti.
Alitoa wito kwa mashabiki wake, Vaddicts, kwa maombi
kwa heshima yake.
"Mke
wangu alimpoteza mama yake kutokana na saratani ya matiti, na niko hapa
nikiomboleza naye ... Sema sala kwa ajili ya mama yake, Vaddicts,"
aliandika.
Huku mashabiki wakisubiri ujio wa albamu yake, Uncle
K anaahidi kuwa zawadi ya kuaga ya kukumbukwa, akionyesha usanii ambao
umemfanya Kizz Daniel kuwa mstari wa mbele wa Afrobeats.
Humu nchini, msanii huyo ni maarufu kwa vibao vyake
kama ‘Cough’ na ‘Buga’.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!