Bradley Marongo, maarufu kama Gen Z Goliath amewashangaza mashabiki wake wengi baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya.

Jamaa huo anayejinadi kama mwanadamu mrefu zaidi nchini Kenya alitetea uamuzi wake akisema kwamba mapenzi hayatambui kabila, mipaka wala rangi ya ngozi.

Alimtambulisha mrembo kutoka Ujerumani kama mpenzi wake na kusema kwamba pamoja watakuwa wanafunzana na kubadilishana utamaduni lakini pia kuweka historia ya kipekee katika maisha yao.

“Mapenzi hayajui mipaka, ninawaleteeni  mpenzi wangu mpya kutoka Ujerumani kwa watu wangu wa ajabu wa Kenya. Hapa tunabadilishana na kuwianisha utamaduni lakini pia kutengeneza kumbukumbu pamoja,” Bradley Mtall aliandika.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Tangazo hili linajiri miezi michache baada ya Marongo kuweka wazi uvumi kuwa alikuwa na mke na kumtelekeza nyumbani kijijini baada ya kupata umaarufu.

Madai hayo yaliibuliwa miezi kadhaa iliyopita alipopata umaarufu na fulusi ambapo mama yake alikuwa wa kwanza kudai kuwa mwanaye amebadilika na hata hawatazami nyumbani.

Hata hivo, akijibu, Bradley alinyoosha maelezo kwamba tatizo kuu ya mama yake ilikuwa kwamba alitaka kila mahali alikokwenda waende na yeye, jambo ambalo alisema halingewezekana.

Marongo alisema kwamba hajaisahau na hawezi kuisahau familia yake, akifichua kuwa alikuwa amemtumia mama yake hela.


Kuhusu mwanamke aliyedaiwa kuwa mpenzi wake, Marongo alisema kuwa hakuwahi muoa na kwamba mrembo huyo alikuwa amemuacha kutokana na ugumu wa maisha.


Jamaa huyo mrefu alimwaga mtama zaidi akisema kuwa mwanamke huyo alianza kujibebisha kwake baada ya umaarufu na fulusi kutua kwake, akimtuhumu kwa kutaka kushusha kitonga kwake na kuteleza kwa ganda la ndizi kimaisha.