
Msanii na mjasiriamali Esther Akoth maarufu kama
Akothee amemkaripia kwa ukali wa simba bukaa aliyejeruhiwa, jamaa mmoja
aliyejaribu kumpa ushauri kuhusu jinsi ya kujibeba akiwa na mpenziwe wake
katika mazingira ya umma.
Mjasiriamali huyo ambaye kwa zaidi ya wiki sasa yuko
nchini Uganda na mpenzi wake Nelly Oaks alichapisha msururu wa picha kadhaa
wakiwa katika hali ya tafrija kwenye mto Nile.
Katika picha hizo, Akothee na Nelly Oaks walikuwa wakicheza densi kwa furaha huku zingine wakiwa wamepakatana na kubusiana kwa mahaba hai.
Mtumizi mmoja wa Facebook alionekana kutofurahishwa
na picha hizo, haswa za wawili hao kubusiana na kumpa Akothee funzo kuhusu
baadhi ya mambo ambayo hafai kuyaonyesha hadharani.
Kwa mujibu wa jamaa huyo, Akothee katika umri wake
hafai kufanya mambo kama ya kubusiana hadharani na mpenzi wakwe, akiitaja kama
tabia mbaya.
Hata hivyo, Akothee naye hakutaka kumweka mfungwa,
alimkabili moja kwa moja akimsuta kwa kuingilia maisha yake.
“Sasa wewe na mimi nani ako na tabia mbaya, I
have been kissed on camera ,wewe bibi yako ushamtia mimba tayari , sasaaa si
hata sisi uwache tutafute mimba style yetu? Nyinyi ni wa usiku muonekane
mchana, sisi ni wa mchana na usiku tuko bisi,” Akothee alimzomea.
Akothee alizama zaidi hadi kuipata picha ya jamaa
huyo akiwa na mwanamke aliyeonekana kama mpenzi wake na kuitumia kumshambulia
zaidi, akimwambia kuwahata yeye kuchapisha picha na mkewe mjamzito hakuna
tofauti na yeye [Akothee] kuchapisha picha akimla denda Nelly Oaks.
“Hivyo wewe unahisi
kuchapisha picha ya mpenzi wake akiwa mjamzito ni tabia nzuri lakini mimi kuchapisha
picha nikimbusu mpenzi wangu ni tabia mbaya? Eeeeh watu waache
kupangie wengine maisha. This is one is a coward cant even hold the wife in
public ,anangoja giza. Weeee mimi siogopi mtu,” Akothee alimfokea.
Hata hivyo, Akothee si mgeni kwa majibu yake makali
kwa watu mitandaoni ambao wanajaribu kuingilia maisha yake au kutaka kumpa
ushauri.
Yeye na Nelly Oaks walirudiana mwaka jana baada ya
kuachana kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Nelly Oaks alirejea katika maisha ya mfanyibiashara
huyo baada ya penzi lake na Mzungu kusambaratika miezi michache baada ya
kufanya harusi iliyotikisa nchi mnamo Aprili mwaka jana.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!