
Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars wametupwa nje
ya mashjindano ya kuwania ubingwa wa Afrika, AFCON, Makala ya 2025 nchini
Morocco baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Zimbabwe.
Mechi hiyo ilikamilika kwa sare ya 1-1 nchini Afrika
Kusini, kumaanisha kwamba Kenya inaungana na Namibia kurudi nyumbani.
Kenya iliwekwa katika kundi J pamoja na Namibia, Zimbabwe
na Cameroon.
Harambee Stars ilihitaji ushindi kabla ya mchezo wao ujao
dhidi ya Namibia na ililazimika kutumaini kwamba Zimbabwe ingepoteza kwa
Cameroon katika mechi yao ya mwisho, lakini matumaini yao yalikatishwa na
Waafrika Kusini.
Harambee Stars walianza vyema huku wakisogeza mpira vizuri
huku wakitafuta bao la mapema ili kuwasumbua wenyeji.
Zimbabwe walipata bao la kuongoza dakika ya 32 kwa shuti la
kwanza lililolenga lango la Tawanda Maswanhise kuachia shuti kali lililompita
Byrne Omondi na kufanya 1-0.
Harambee Stars ilipata bao lao la kusawazisha dakika ya 52
Jonah Ayunga alipotumia vyema makosa ya safu ya ulinzi baada ya kipa Mzimbabwe
kumwaga mpira, na hivyo kumruhusu Ayunga kuukwaa mpira uliorudi kabla ya beki
wa Warriors kuuondoa nje ya mstari.
Matumaini ya Kenya kushiriki AFCON ni hadi mwaka 2027 ambapo
watakuwa waandalizi wakishirikiana na Uganda (ambao tayari wamefuzu kwa Makala ya
2025) pamoja na Tanzania.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!