Muigizaji Jacky Matubia amefichua kwamba maisha yake ya utotoni yalikuwa na kiwewe kisichoweza kuelezeka kutokana na tofauti kati ya wazazi wake.

Mama huyo wa mabinti 2 alisema kwamba alimchukia mama yake sana baada ya kugundua kwamba alimzaa katika hospitali ya kujifungua kina mama ya Pumwani na kumtelekeza huko kwa miezi 3.

Matubia alisema kwamba maisha yake yote ya utotoni yalikuwa ya kutojikubali, jambo ambalo linamtatiza mpaka sasa.

Ilikuaje?

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kwa mujibu wa muigizaji huyo, kulikuwa na tofauti za kutoelewana kati ya babake na mamake, jambo ambalo alisema kuwa mpaka sasa hawajahi zungumza wala kuonana ana kwa ana.

“Niliishi London kwa miezi 6 na babangu kabla ya kurudishwa kwa mamangu Kawangware. Mama alipigana sana kunilea. Mimi binafsi nilikuwa namchukia sana mamangu. Nilikuwa najiuliza mbona unilete duniani kama ulikuwa unajua nitakuja kuteseka,” Matubia alisema.

“Mamangu na babangu hawazungumzi mpaka leo hii nikiwa na umri wa miaka 34. Hawajawahi onana. Kutojikubali kwangu kulianza wakati mamangu alinizaa. Aliniacha Pumwani kwa miezi 3 bila mlezi kwa sababu aliambiwa mimi ni sura mbaya. Nilikuwa mweusi na nywele nyingi,” aliongeza.

‘Hivyo ni kama nilizaliwa tu kwa kujikataa na limekuwa ni jambo ndani yangu.”

Akiwa katika shule ya upili, Matubia alisema hapo ndipo alianza kujitambua kwa sababu alipelekwa katika shule ambayo iliwiana na hali ya uchumi ya mama yake.

Matubia alisema kuwa baada ya kumaliza kidato cha nne, alipata kazi yake ya kwanza ya uigizaji kwenye Tahidi High ambapo mshahara wake wa pili alihama kutoka kwa mamake Kawangware na kuishi Imara Daima.

Akizungumzia kuhusu alichokifunza kutoka maisha yake ya utotoni, Matubia alisema yeye si bahili wa kutumia pesa, akisisitiza kwamba asingependa kuwakuza wanawe katika maisha sawia na yale aliyopitia.

“Nisingependa kurudi kule nilikokuwa. Nisingependa hata kidogo kuwalisha wanangu ugali na chai pekee. Na ndio maana ninafanya kazi kwa bidii. Nimeamua kupumzika itakuwa ni mbinguni;” alisema.