
Msanii wa miziki ya kizazi kipyua kutoka Tanzania,
Harmonize amefichua kwamba tathmini ya haraka katika maisha yake ya ukubwa,
amebaini kwamba wapenzi wake wote wamekuwa ni wa dini ya Kikristo.
Msanii huyo wa lebo ya Konde Gang alisema kwamba
licha ya yeye kuwa Muisalmu, lakini hajawai kuwa katika penzi la mrembo Muislamu,
akisema kwamba warembo Wakristo wanaitaka ngome yake kwa udi na uvumba; jino na
ukucha.
Alisema kwamba kwa sasa baada ya penzi lake
kusambaratina na Poshy Queen, anataka kujaribu bahati yake katika mapenzi kwa
mara ya mwisho, ila safari hii angependa kupendana na mrembo Muislamu.
Kama kawaida, Harmonize alisema vigeoz vyake vipo
pale pale kwamba lazima mrembo huyo Muislamu awe amebarikiwa kwa ‘zigo nene’.
“Kuna jinsi watoto wa Yesu wanalitaka hili jimbo. Yaani
leo ndio nimegundua sijawahi kuwa katika penzi la hakika na binti yeyote wa
Kiislamu maisha yangu yote. Au shida inaanzia hapo? Au labda mke wangu yuko
uko? Tafadhali nitafutie mrembo wa Kiislamu, huwezi jua. Sharti awe
amefungasha, mashine iwepo tafadhali,” aliwaomba wafuasi wake.
Msanii huyo tangu alipopata umaarufu kwenye tasnia ya
muziki wa Bongo Fleva mnamo mwaka 2014, aliingia katika mahusiano na muigizaji
Jackline Wolper kabla ya kuchumbiana na Muitaliano Sarah Michelloti.
Baadaye alipendana na Fridah Kajala ambaye waliachana
na kurudiana mwaka mmoja badae kabla ya kuachana tena miezi sita tu baada ya
kumvisha pete ya uchumba.
Alikawia kwa muda kabla ya kujaribu bahati yake ya
penzi kwa mrembo Poshy Queen ambaye wameachana wiki kadhaa zilizopita.
Katika mahusiano haya yote, kitu kimoja kilisalia
kuwa kile kile kwamba wote ni warembo wa dini ya Kikristo.
Sasa baada ya kufunguka macho na kuona hilo,
Harmonize amehisi kwamba kuchumbiana na warembo wa dini ya Kikristo hali ya
kuwa yeye ni Muislamu huenda ndicho kizingiti kikubwa ambacho husababisha penzi
lake kukatishwa ghafla hata kabla ya kumaliza mwaka.
Amesema fikira na mawazo yake yamemtuma kuamini
kwamba pengine Mungu amemhifadhiwa wa ubavuni mwake katika dini ya Kiislamu na
yeye tamaa za kidunia zinamuongoza tu katika mitego ya warembo wa Kikristo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!