Mwanasosholaiti Huddah Monroe amejitokeza wazi na kukiri kwamba anajionea huruma kwa kile alichokitaja kuwa ni kumpigia rais Ruto debe kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 2022.

Kupitia Insta story yake, Monroe alisema kwamba anajuta kitendo hicho akidai kuwa rais amefeli katika maazimio yake mengi aliyowaahidi Wakenya katika manifesto yake.

Mwanasosholaiti huyo alisema kwamba mtambo wa KRA uko na hitilafu kila mara kuifanya kuwa vigumu walipa ushuru kutekeleza wajibu wao, akiwashauri Wakenya kutompa ‘mtoto wa maskini’ wajibu wa kuwaongoza tena.

“Mitambo ya KRA ina hitilafu kila mara, Kenya imekuwa kama kichaka kikubwa. Ni kijiji tu ndichi kinastahili kuwa na matatizo kama haya. Sasa mmejua, msiwahi kumpa uongozi mtoto wa maskini tena. Pengine tu kama amejenga biashara yake iliyostawi,” Monroe alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Niliweka ubashiri mbaya! Mimi ni miongoni mwa watu waliompigia debe bila aibu,’ Huddah aliongeza.

Katika siku za hivi karibuni, mwanasosholaiti huyo ambaye mara nyingi hayuko nchini amekuwa akijiingiza katika masuala ya uongozi wa Kenya, kinyume na awali ambapo alikuwa amejikita katika kutangaza biashara zake kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Hii si mara ya kwanza ambapo sosholaiti huyo alikosoa utawala wa Rais Ruto.

Huku kukiwa na kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula mnamo Septemba 2023, Huddah alionyesha kutoridhika kwake, akidai kwamba Ruto atakumbukwa kama rais mbaya zaidi wa Kenya.

Ikumbukwe Monroe alikuwa mmoja wa watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii ambao walionyesha wazi uungaji mkono wao kwa Ruto tangia mwaka wa 2017 akiwa naibu rais wa aliyekuwa rais, Uhuru Kenyatta.

Wakati Ruto alishinda katika uchaguzi wa urais wa 2022, Huddah alikuwa miongoni mwa wa kwanza kusherehekea, akishiriki picha nyingi za kiongozi wa taifa akichapisha picha zake kwenye Instagram, ambapo alimtaja kama "rais wangu."

Alionyesha hisia mpya ya fahari ya kitaifa.

“Ninajivunia kuwa Mkenya kuanzia leo. Afrika inastahili viongozi wenye nguvu, wenye akili timamu, vijana. Kenya imefanya mabadiliko kwa Afrika. Nitabeba bendera na pasipoti yangu kwa fahari kuanzia leo. Ninatoka Kenya, nchi kubwa zaidi barani Afrika!” Alisema.