Heaven Bahati, binti wa kwanza wa maceleb Diana Marua na Kevin Bahati Kioko amefichua mipango yake ya ni lini ataondoka katika nyumba ya wazazi.

Akizungumza na wazazi wake wakati aliwaandalia zawadi ya kuwashukuru kwa malezi, binti huyo aliwaambia Bahati na Diana kwamba mpango wake ni kuondoka chini ya mbavu zao afikapo umri wa miaka 21.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 7 alisema kwamba kabla hajaondoka, atachukua picha nzuri za wazazi wake zitakazosalia naye kama kumbukumbu ya milele katika moyo wake ili asije akawasahau.

“Siwezi kuwasahau hata wakati nitaenda katika nyumba nyingine. Ninapanga kuenda katika nyumba yangu nikifikisha umri wa miaka 21.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Lakini nitakuwa ninawaweka moyoni milele, nitachukua picha zenu nzuri na nitazitunza kwangu muda wote. Nitafanya hivyo kama njia moja ya kuhakikisha siwapotezi katika moyo wangu,” binti huyo alieleza kwa hisia.

Binti huyo mrembo aliwamiminia wazazi wake sifa, akisimulia jinsi wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisaha familia yao hailali njaa.

“Ninawathamini kwa sababu nyinyi ni wazazi 2 mnaofanya kazi kwa bidii kulisha familia ya watoto 5. Mama anakuwa kila wakati akifanya vitu vingi vizuri kwa ajili yetu, hata kama tunakosea, tunafoka. Lakini pia baba anafanya kazi sana, anasafiri sana mpaka kwa muda sasa hatujakuwa tukimuona kwa sababu amekuwa safarini akitusaidia kupata pesa,” Binti Heaven alisema.

Hii si mara ya kwanza kwa binti huyo kuwapunga wazazi wake kwa mawazo yake kuhusu maisha yake ya kibinafsi.

Itakumbukwa mwezi Julai mwaka huu, Heaven Bahati alimuacha mamake kinywa wazi baada ya kumuonyesha pete yake vya uchumba, akiwa na umri wa miaka 6.

Diana alikuwa amejiandaa kutoka kukutana na baadhi ya mashabiki wake na kusherehekea kupokezwa Kitufe ch Dhahabu kutoka YouTube baada ya kufikisha wafuasi milioni 1 mapema mwezi Februari mwaka huu.

Diana alikutana na bintiye nje na kumuonesha pete zake mbili akimfafanulia bintiye kwamba moja ni ya urembo na nyingine ni ya kuonyesha uhusiano wake wa kimapenzi na mumewe, Bahati Kioko.

 Kwa mshangao, Heaven pia alimuonyesha mama yake pete mbili kwenye vidole vyake mkononi na kusema moja ni ya urembo na nyingine ni kwa ajili ya ‘mumewe’, akisema kwamba yuko tayari kuolewa siku wazazi wake watamruhusu kutoka bila kuomba ruhusa.

“Kwa sasa nimeolewa na watu wawili,” Heaven Bahati alisema kabla ya mamake kumkatisha na kumwambia kwamba angependa aje kuolewa na mtu mmoja baadae mbeleni.