Msanii wa gengetone na Mugithi, Peter Miracle Baby ametoa jibu saa chache baada ya kuonekana kwenye klabu ya starehe akitumbuiza.

Msanii huyo alikuwa mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa kwenye klabu, miezi kadhaa baada ya kuweka wazi kwamba alikuwa ameanza safari yake ya uokovu.

Akijitetea kurudi katika maisha ya zamani licha ya kudai kuokoka, Miracle Baby alinukuu Biblia akisema kwamba watu hawafai kumweka kwenye mizani kutaka kujua kwa nini alionekana klabuni.

Msanii huyo alisema kuwa vipaji vyote vinatoka kwa Mungu bila kubagua cha injili au cha tumbuizo la dunia, akisema kwamba anataka kutumia kipaji alichopewa na Mungu kwa njia sahihi ili asije kukosa majibu machoni pa Mungu siku ya Kiama.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Nimeona watu wengi wakihoji kuhusu mimi. Nilirudi kwenye muziki wa kidunia ndio nimerudi na nataka nizungumzie hicho kipaji kimetolewa na Mungu na ipo siku ataniuliza nilikupa kipaji ulichofanya nacho ni kipi?” Miracle Baby alisema.

Kijana huyo alisema kwamba hahitaji kuambiwa chochote cha kufanya na kipaji chake, akisisitiza kwamba ataendelea kumsifu na kumtukuza Mungu kwa njia yake aijuayo mwenyewe.

“I'll still serve the Lord in my own way ..kitu ingine niko na familia inanitegemea I need to work so that niweze kuwapea basic needs e.t.c so stop judging me coz wewe mwenye unani judge, uko na makosa kama hujui ndio hii,” alifoka huku akinukuu Biblia.

“Mathayo 7 : "Msihukumu, msije ninyi mtahukumiwa; kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo mtakavyohukumiwa; na kwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa. ukitazama kibanzi kwenye jicho la ndugu yako, na boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe huiangalii?” alinukuu.

Msanii huyo alikuwa mgeni wa hospitali kwa miezi kadhaa tangu Januari mwaka huu ambapo alifanyiowa upasuaji mara kadhaa, kama alivyoeleza mpenzi wake Carol Katrue.

Baada ya kusaidiwa kutoka hospitalini, Miracle Baby alitangaza kwamba Mungu amemtoa mbali na kwamba ataanza kumtumikia kueneza injili yake.


Miracle Baby kwa wakati mmoja hata alisema kwamba angeanza kutumikia Mungu kwa nyimbo za injili kabla ya kujenga kanisa na kuanza kuhubiri kama mchungaji mkuu.