Kocha wa muda Ruud van Nistelrooy mnamo Jumatatu jioni aliondoka katika klabu ya Manchester United kufuatia kuwasili kwa Ruben Amorim na timu yake mpya ya ukufunzi.
Hii ilitokea baada ya mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 48 kutopewa nafasi katika timu ya Ruben Amorim. Alikuwa amechukua mikoba ya Old Trafford kwa muda baada ya kocha mwenzake Erik ten Hag kufutwa kazi mwezi uliopita.
Amorim, 39, hata hivyo hataingia kazini hadi baadaye wiki hii kutokana na suala la visa, lakini yeye na timu yake waliojiunga naye kutoka Sporting Lisbon walisafiri kwa ndege kuelekea Manchester mnamo Jumatatu kabla ya mechi yake ya kwanza kwenye usukani dhidi ya Ipswich Town baadaye mwezi huu.
"Manchester United inaweza kuthibitisha kwamba Ruud van Nistelrooy ameondoka katika klabu. Ruud alijiunga tena msimu wa joto na amechukua jukumu la kuinoa timu kwa mechi nne zilizopita kama kocha mkuu wa muda," taarifa ya Manchester United ilisoma.
Ilisomeka zaidi, "Ruud ni, na daima atakuwa, gwiji wa Manchester United. Tunashukuru kwa mchango wake na jinsi ambavyo amekuwa akishughulikia jukumu lake kwa muda wote akiwa na klabu. Atakaribishwa sana Old Trafford kila wakati .”
Mchezaji huyo wa zamani wa Man United aliondoka pamoja na makocha wengine waliofanya naye kazi.
Rene
Hake, Jelle ten Rouwelaar na Pieter Morel pia wameondoka na tunawatakia kila la
heri kwa siku zijazo. Tutathibitisha muundo kamili wa ukufunzi wa kikosi cha
kwanza cha wanaume kwa wakati ufaao," klabu hiyo ilisema.
Hata hivyo, kiungo wa zamani wa United, Darren Fletcher, atasalia katika nafasi yake ya ukocha na kuendeleza kuwa kiungo kati ya kikosi cha kwanza na akademi.
Van Nistelrooy, ambaye alijiunga na United kama kocha msaidizi mwezi Julai kwa mkataba wa miaka miwili, alifanikiwa kushinda mara tatu na sare katika mechi zake nne wakati akiwa kocha wa muda.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!