Mwanaharakati wa elimu ya kiraia, Morara Kebaso ameonyesha sura nzuri ya mkewe kwa mara ya kwanza kwa mashabiki na wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Kebaso, akisherehekea ndoa yake, alifichua kwamba amedumu kwenye ndoa na mrembo huyo kwa miaka 6 sasa.

Akizungumzia kuhusu uzoefu wake kwenye ndoa, kiongozi huyo wa chama cha INJECT alieleza kwamba japo amekaa katika ndoa kwa miaka 6, kwake kila siku huhisi kama ni mpya katika ndoa yake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Apataye mke apata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana. Nina miaka sita kwenye ndoa sasa na kila siku ni siku mpya. Siwezi hata kusema nina uzoefu. Ninajifunza kila siku,’ Kebaso alisema.

Wiki chache zilizopita, Kebaso alisherehekea kufikisha umri wa miaka 29, kumaanisha kwamba alifunga ndoa akiwa katika umri wa miaka 23.

Alipata umaarufu kote nchini kupitia ukosoaji wake wa kuchekesha wa miradi ya serikali iliyokwama kote nchini.

Hivi majuzi, Kebaso aliapa kuendelea na ukosoaji wake dhidi ya serikali licha ya upinzani ambao amekuwa akikabiliana nao siku za hivi karibuni.


 


Morara amelazimika kukabiliana na ukosoaji, haswa kutoka kwa mtandao wake, ambao wengine wamemwita tapeli baada ya kuanza kuomba pesa za kuwezesha harakati zake kote nchini.