Msanii na mwanaharakati wa kisiasa maarufu Kasmuel McOure amejiunga na chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kinachoongozwa na Raila Odinga.
Katika taarifa Jumapili, , Kasmuel ambaye alijizolea umaarufu zaidi wakati wa maandamano ya vijana alisema chama hicho sasa kiko tayari kufufua ligi za vijana na wanafunzi kote nchini. Hii ilikuwa baada ya mkutano na mwenyekiti wa chama hicho na ambaye ni Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga
Kasmuel aliendelea kusema kuwa ODM ndicho chama pekee kinachounga mkono watu katika Afrika Mashariki na Kati.
Aidha mwanaharakati huyo alitoa wito kwa vijana kujiunga na chama hicho akisisitiza kuwa ni vuguvugu pekee la kisiasa linalosukuma nchi ambayo kila mtu anaweza kuishi kwa utu.
"Ikiwa uko tayari kujiunga na vuguvugu kubwa la kisiasa kwa ajili ya Kenya ya haki, ya kidemokrasia ambapo kila mtu anaweza kuishi kwa heshima, zingatia @TheODMparty - chama kikubwa zaidi cha wafuasi katika Afrika Mashariki na Kati!
“Tunafufua Ligi za Vijana na Wanafunzi na tunatoa wito kwa vijana wa Kenya walio na shauku kusaidia kuunda maisha yetu ya baadaye. Simama nasi! Asante, mwenyekiti wa chama @gladyswanga, kwa imani yako na kutukaribisha wikendi hii,” Kasmuel alisema.
Kasmuel alisema pamoja na watu wengine watakuwa wakienda katika harakati za kuwapata wasomi na wasio na elimu wajiunge na chama hicho.
Pia atashiriki katika kuwafanya vijana
kujisajili kuwa wanachama wa ODM.
Gavana Wanga kwa upande wake alisema mustakabali wa ODM ni wa vijana mahiri kama Kasmuel Mc Oure.
“ODM ni chama cha siku zijazo na mustakabali wa ODM uko mikononi mwa vijana wetu. Gen Z wetu, na Gen Alphas, ndio wanakuja na ndiyo maana tunataka ushirikishwaji mkubwa wa vijana mahiri kama (Kasmuel) Mcoure,” alisema.
Hatua ya kujiunga na ODM inajiri wiki chache baada ya Kasmuel kufanya mkutano na aliyekuwa Waziri Mkuu na kiongozi mwanzilishi wa chama cha ODM, Raila Odinga.
Kasmuel ni mmoja wa wanaharakati vijana ambao walikuja kuwa uso wa maandamano ya Gen Z nchini Kenya mapema mwaka huu, kufuatia kupitishwa kwa Mswada wenye utata wa Fedha wa 2024 na Wabunge.
Kijana huyo alikuwa miongoni mwa walioongoza vuguvugu la kuipinga serikali mitandaoni na mitaani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!