KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Novemba 10.  

Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja unusu  jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kakamega, Kisumu, na Kiambu.

Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za barabara za Rangwe na Kampala zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Eneo la Matawa katika kaunti ya Kakamega litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja unusu jioni.

Sehemu za mtaa wa Milimani na eneo la Kano katika kaunti ya Kisumu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu za maeneo ya Kiandutu, Kahawa Bora, Chania Feeds na Capwell zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.