Siku ya Jumamosi jioni, meneja wa soka mwenye sifa ya juu Pep Guardiola alipoteza mechi ya nne mfululizo kwa mara ya kwanza katika taaluma yake ya ukocha.

Licha ya kufunga bao la kwanza, Man City ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Brigton & Hove Albion katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa The American Express Community mwendo wa saa mbili unusu jioni.

Mshambulizi matata Erling Haaland alianza kuifungia City katika dakika ya 23 kabla ya Joao Pedro kuisawazishia Brighton kunako dakika ya 78, huku Matt O'Riley akiifungia Seagulls bao la ushindi katika dakika ya 83.

Kipigo cha Brighton cha Jumamosi jioni kilifanya kuwa vipigo vinne mfululizo kwa vijana wa Pep Guardiola katika mashindano yote. Hawajashinda mechi yoyote kati ya nne zilizopita, na hii ni mara ya kwanza inatokea kwa meneja huyo mwenye umri wa miaka 53.

"Inaweza kutokea mara moja katika maisha, sivyo? Daima kuna mara ya kwanza," Pep Guardiola alisema kuhusu kushindwa kwake kwa mara ya nne mfululizo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hata hivyo alieleza imani yake kuwa timu yake itarejea na kuendelea kushinda michezo kama walivyofanya katika siku za huko nyuma.

"Tumepoteza michezo miwili kwenye Ligi Kuu na lazima tubadilishe, turudi kwenye ushindi. Tuko katika nafasi ambayo tuko kwenye meza,” alisema.

Akizungumzia mechi dhidi ya Brighton, alibainisha kuwa vijana wake walicheza vizuri lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kupata ushindi.

Alizungumzia kutokuwa na mwendo sawa kuwa tatizo kuu lakini aliahidi matokeo bora kutoka kwa timu yake baada ya mapumziko ya kimataifa yanayokuja.

"Leo tulicheza vizuri sana katika kipindi cha kwanza lakini hatukuweza kumaliza mchezo. Hatukuwa thabiti kudumisha mchezo wetu na umakini wetu na kucheza kwa nguvu kwa dakika 90. Kiwango tunachocheza ni nzuri sana katika nyakati fulani. lakini hatuwezi kuendelea kwa muda mrefu,” alisema.

Aliongeza, "Nina uhakika wachezaji watakaporudi (baada ya mapumziko ya kimataifa) na tukifanya sifa za kibinafsi kwenye timu, tutarejea."

Licha ya hali mbaya ya hivi majuzi, Man City bado wako katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 23 kati ya michuano ya Ligi 11 waliyocheza.