Aliyekuwa seneta wa kuteuliwa Millicent Omanga ameteuliwa kuwa mwanachama wa bodi ya Hazina ya Ruzuku ya Mamlaka za Mitaa (LAP FUND).
Samuel Kariuki Maina na Beatrice Kones pia waliteuliwa katika bodi hiyo.
Watatu hao watahudumu kwa miaka 3, kuanzia Novemba 8, 2024. Uteuzi huo ulifanywa na Waziri wa Hazina John Mbadi mnamo Ijumaa.
“Katika kutekeleza mamlaka aliyopewa na kifungu cha 5 (1) (a) cha Sheria ya Mfuko wa Ruzuku ya Serikali za Mitaa, kama kikisomwa pamoja na kifungu cha 51 (1) cha Sheria ya Tafsiri na Masharti ya Jumla, Waziri wa Hazina ya Taifa na Uchum ameteua— Samwel Kariuki Maina, Beatrice Kones, Millicent Nyaboke, kuwa wanachama wa Bodi ya Hazina ya Ruzuku ya Mamlaka za Mitaa, kwa miaka mitatu (3), kuanzia tarehe 8 Novemba 2024,” Notisi ya Gazeti ilisema kwa sehemu.
LAP FUND inadhibitiwa na Mamlaka ya Mafao ya Kustaafu (RBA), na ni mojawapo ya mipango ya zamani zaidi ya mafao ya kustaafu nchini Kenya na ina zaidi ya wanachama 70,000. LAPFUND ni Shirika la Serikali lililoanzishwa mwaka wa 1960 kwa Sheria ya Bunge.
Uteuzi mpya wa Omanga unakuja siku chache baada ya kukataa uteuzi wa Rais William Ruto katika Tume ya Mito ya Nairobi, akitoa sababu za kibinafsi.
Seneta huyo wa zamani aliteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, ambaye uteuzi wake ulipingwa kisheria.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!