Rais wa Ghana anayemaliza muda wake Nana Akufo-Addo anakabiliwa na mzozo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuzindua sanamu yake alipokuwa katika ziara ya Ukanda wa Magharibi mwa nchi hiyo.
Sanamu hiyo imesimikwa kwa heshima ya mipango ya maendeleo ambayo Rais amesimamia akiwa madarakani, Waziri Kwabena Okyere Darko-Mensah alisema.
Lakini Waghana wengi wamekuwa wakidhihaki usimikwaji wake nje ya hospitali katika jiji la Sekondi – wanaiona kama njia ya "kujitukuza".
"Watu wa Ukanda wa Magharibi wanastahili jambo bora zaidi ya maonyesho ya kujionyesha ," Mbunge wa upinzani Emmanuel Armah Kofi-Buah alichapisha kwenye X.
Akufo-Addo, ambaye atang'atuka madarakani Januari baada ya mihula miwili madarakani, amejigamba kuwa ametimiza asilimia 80 ya ahadi zake kwa Waghana.
Alizindua sanamu hiyo iliowekwa mbele ya hospitali ya Effia-Nkwanta ya jimbo la Sekondi , Jumatano wakati wa ziara yake ambayo imepewa jina la "safari ya shukrani".
Katika hafla hiyo, Darko-Mensah, ambaye anasimamia Kanda ya Magharibi, aliangazia miradi kadhaa muhimu iliyoanzishwa chini ya rais.
Lakini sanamu hiyo imezua wimbi la ukosoaji, huku baadhi ya Waghana wakihoji umuhimu wake wakati miradi kadhaa muhimu haijakamilika.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!