Aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa Agosti 2022, George Wajackoyah kwa mara nyingine amewakumbusha Wakenya kuhusu manifesto yake kuelekea uchaguzi huo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Wajackoyah amewakumbusha Wakenya kwamba aliwasisitizia mara si moja kuhusu faida na umuhimu wa kuwa wafugaji wa nyoka lakini wengi hawakumsikia wala kutilia maanani wosia wake.

Msomi huyo wa sheria alionyesha picha za nyoka akisema kwamba kilimo cha nyoka kwa sasa kina faida nyingi katika kila pembe ya dunia, na kusikitika ni kwa nini Wakenya hawakumsikia.

Wajackoyah alieleza kwamba nyama ya nyoka kilo moja kwa sasa inauzwa kwa hadi dola 30 sawa na shilingi 3,900 pesa za Kenya.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Niliwaambia Wakenya kwamba kufuga nyoka kungesaidia watu wetu kwa njia mpya ya mapato. Nyama ya nyoka ni kitamu katika Mashariki ya Mbali. Kilo moja ya nyoka wa kitropiki ni $30,” Wajackoyah alisema.

Wakili huyo msomi alielezea kwamba kando na nyama ya nyka kuwa na faida kubwa, pia jamii za Wachina hutumia mifupa yake kuchochea mihemko na msisimko wa kufanya mapenzi.

Alisema pia kuwa ngozi ya nyoka ndio inapendelewa zaidi katika kutengeneza mikoba lakini pia sumu yake ni ghali sana ambayo inauzwa kwa hadi dola elfu sita, sawa na Sh 773,000 za Kenya.

“Wachina wanatumia mifupa ya nyoka kushawishi Nyege. Ngozi hutumiwa kutengeneza viatu vya ngozi na mikoba. Kulikuwa na soko la Italia. Kisha uchimbaji wa sumu. Gramu moja ni $6000.” Alisema.

Mwanasiasa huyo alizidi kufafanua faida za ufugaji wa nyoka akisema kwamba nyoka wakifugwa pia watavutia utalii lakini pia uganga, akionyesha mfano wa nyoka aliyemilikiwa na mganga mmoja maarufu.

“Kutumia nyoka kwa uganga na kukimbia usiku na vile vile inaweza kuvutia Usanii na utalii. Nyoka huyu alikuwa wa mwenyekiti wa wachawi pale Indangalasia. Kundi hili linajumuisha vikongwe wanaoaminika kuwa wachawi katika maeneo yani warogi. Huyu aliuawa asubuhi ya leo na mabaki yamezuiliwa katika mto Nzoia. Ni upotevu ulioje!” Wajackoyah alisikitika.