Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee ameendelea kumwagia sifa kemkem mpenzi na meneja wake Nelly Oaks.

Siku ya Jumatano, mama huyo wa watoto watano aliandika ujumbe mrefu kumthamini mpenzi huyo wa maisha yake na kueleza jinsi amekuwa akimuunga mkono.

Akothee alizungumza kuhusu jinsi Nelly Oaks alivyojitolea kuwa naye wakati wa hafla ya kuhitimu  ya kwanza kabisa katika Akothee Academy licha ya kuwa amechoka na hakuwa anajisikia vizuri.

“Ninataka kumpongeza mume wangu, Bw. Mwenyekiti wa Akothee Academy, kwa usaidizi wa ajabu ambao ameonyesha. Leo, nilitambua jinsi ahadi yake ilivyo thabiti, kwangu kama mke wake na kwa kampuni,” Akothee alisema.

Msanii huyo aliyezingirwa na drama nyingi maishani alisimulia jinsi wiki moja kabla ya sherehe ya kuhitimu ilivyokuwa na shughuli nyingi kwao hivi kwamba akawa na wasiwasi ikiwa wangefika kwenye hafla hiyo.

“Kilichonigusa zaidi ni jinsi (Nelly) alivyosukuma, licha ya kuwa amechoka na kutojisikia vizuri. Usiku huo, alipokuwa akipambana na kichefuchefu, niliogopa—sikujua kama angemaliza, lakini alifanya hivyo. Tulipanda ndege hadi Kisumu kama Riddick, tukiwa tumelala kwa shida. Nilikuwa na wasiwasi wa kumpeleka kijijini katika jimbo hilo, lakini nguvu zake zilinifanya niendelee,” alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Akothee alifichua kuwa licha ya kutokuwa katika hali nzuri, mpenzi wake alikaa shuleni hadi hafla hiyo ilipokamilika.

"Licha ya hali yake, alipigania kuwepo na kusaidia safari ya shule, hata kwa gharama ya afya yake. Sherehe ilipokamilika, alinikaribisha tena ndani ya gari kwa tabasamu mchangamfu na lililochangamsha,” alisema.

Tukio hilo lilipoisha, Nelly alimpongeza mwimbaji huyo kwa jinsi shule yake inavyokua na kumhakikishia kuwa itakuwa kubwa zaidi.

“Ishara hii iligusa sana moyo wangu. Sasa unaelewa ni kwa nini hata tunapokosea tunasameheana—hata sisi ni binadamu tu,” alisema.

Tangu siku hiyo, Nelly amejionyesha kuwa mmoja kati ya milioni, na nitampa upendo na umakini wote anaostahili. Yeye ndiye kila kitu kwangu. Sina mtu mwingine ila yeye,” alisema.

Katika ujumbe huo mama huyo wa watoto watano pia alidokeza kuhusu kufunga ndoa rasmi na Nelly na kuzaa naye.

“Tupigie makofi na mshone vitenge. Na nguo za Baby shower,” alisema