
Siku moja baada ya uchaguzi wa Marekani kukamilika na Donald Trump kutangazwa mshindi, video imeibuka mitandaoni ya Mmarekani mmoja akifichua jinsi Babu Owino alichangia katika ushindi wa Trump.
Katika video hiyo, Mmarekani huyo alifichua kwamba yeye alikuwa analenga kumpigia kura Kamala Harris lakini baada ya kuona video ya Babu Owino akimpigia debe Trump, ilimbidi abadili nia yake.
Kijana huyo alikiri kwamba alimpigia Trump kura kutokana na ushawishi wa Babu Owino, huku akimshukuru mbunge huyo wa Embakasi Mashariki kwa kusababisha kura yake kuelekea katika mrengo wa ushindi.
"Babu Owino Embakasi Mashariki, ni furaha kabisa na heshima ya kibinafsi kuelewa kwamba uliidhinisha kibinafsi Donald Trump kuwa rais. Binafsi, ninaona kuwa ni heshima kubwa kwamba ikiwa kiongozi wa kigeni wa nchi ambaye anaweza kuifanya Kenya kuwa kuu tena atamwidhinisha mmoja wa wagombeaji wakuu katika historia ya Marekani,” mpiga kura huyo alisema.
"Kwa kweli nilikuwa nikifikiria kumpigia kura Kamala, lakini nilipoona kwamba uliidhinisha Trump nilimwambia Kamala, 'Umefutwa kazi. Toka ofisini kwako.’ Tunarudisha Amerika,” akasema.
Akichapisha picha hiyo kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Babu Owino alishukuru mpiga kura huyo wa Marekani kwa kushawishika naye.
“Nawashukuru sana Wamarekani ambao walikubali na kuthamini uidhinishaji wangu kwa Rais Trump. Nitakapokwenda Marekani bila shaka nitakutana na bwana huyu ambaye alibadili mawazo yake ya kumpigia kura Trump baada ya kumuidhinisha hadharani Trump.Embakasi East Republic to the world,” Owino alisema.
Donald Trump alimshinda Kamala Harris katika uchaguzi wa rais wa Novemba 5, 2024, akishinda Chuo cha Uchaguzi na kura maarufu.
Chuo cha Uchaguzi kina wapiga kura 538. Idadi kubwa ya kura 270 za uchaguzi zinahitajika ili kumchagua Rais wa Marekani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!