Mjasiriamali Sarah Kabu amewashauri kina dada katika ndoa, akiwasisitizia kwamba kigezo cha mwanamume kutoka nje ya ndoa kisiwe cha pekee kuwahamisha kutoka katika ndoa zao.


Katika klipu hiyo iliyoibuliwa mitandaoni, Sarah alikuwa anazungumza kwenye runinga ya KTN Home ambapo alishauri kwamba wanaume kuchepuko halifai kuwa jambo pekee la kuwakera wanawake na kuwafanya kuvunjika katika ndoa.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Ningependa tu kuwadokezea wanawake kwamba haya mambo hutokea. Kila wakati ninapata content ynye naweza chanua wanawake, huwa muda wote naipakuwa kwao.”


“Siku hizi mimi huwaambia wanawake, kwa kweli kuchepuka hakufai kuwa moja ya sababu yetu kuwaacha wanaume au kuanza kuwa na wasiwasi kuhusu wanaume wetu. Hebu acha tuwe na mashaka kuhusu vitu vingine vikubwa kuliko kuwa na mashaka iwapo anachepuka au la,” Sarah Kabu alisema.


Sarah ambaye amedumu kwa ndoa kwa miaka kadhaa na mpenzi wake, CEO wa Bonfire Adventures, Simon Kabu alisema kwamba katika uzoefu wake kwenye ndoa, mwanamke ukijifanya huna mashaka iwapo mume wako anachepuka, mwanamume mwenyewe ndiye huanza kuingiwa na wasiwasi.


“Wakati tunaacha kuwa na wasiwasi, kwa kweli wao wenyewe sasa ndio huanza kuingiwa na wasiwasi. ‘inakuaje hunifuatilii’ na mambo kama hayo. Wanaume muda wote huwa wanataka kutuona tukiwafuatilia, tukiwaombea, hivyo ninawaambia wanawake tucheze chini kidogo,’ alishauri.


Aliongeza ushauri akiwaambia wanawake kuwa na mazoea ya kuwaacha wanaume kuwa jinsi waliumbwa kuwa bila kuwawekea vikwazo vingi katika maisha, kisha kakuoa.


‘Hebu na tuwaache wanaume kuwa jinsi walivyoumbwa kuwa.”