
Takriban wafanyakazi 200 wamenaswa katika msako dhidi ya watu walio na karatasi ghushi za masomo Bungeni.
Mwenendo huo unaonyesha uozo mkubwa wa maadili na ufisadi katika ajira za serikali ambao bado haujafichuliwa na Tume ya Utumishi wa Umma - mwajiri wa watumishi wa umma.
Gazeti la The Star limebaini kuwa zoezi hilo lililoamriwa na Tume ya Utumishi wa Bunge zaidi ya mwaka mmoja uliopita limewapiga msasa watumishi waandamizi na wa chini. Ufichuzi huo umezua hofu katika Bunge huku kukiwa na hofu kwamba maafisa zaidi wanaweza kuathirika katika siku na wiki zijazo. Katika ukaguzi huo,
Bunge linathibitisha uhalisi wa vyeti vya KCPE, KCSE, diploma, shahada na uzamili vinavyomilikiwa na wafanyikazi wake.
Kwa sasa, ukaguzi huo umelenga wafanyikazi kwenye orodha ya malipo ya PSC, huku wadadisi wakiashiria kuwa hivi karibuni itaachiliwa kwa wale wanaofanyia kazi wabunge katika afisi za maeneo bunge.
Takriban watu 1,300 wako kwenye orodha ya malipo ya PSC. Hii haijumuishi wafanyikazi katika ofisi za maeneobunge ya wabunge.
Miongoni mwa maafisa ambao tayari wamenaswa katika kashfa hiyo ghushi ya kitaaluma ni pamoja na wakurugenzi wakuu na manaibu wakurugenzi.
Ni pamoja na wafanyikazi wa kudumu na walio kwenye mikataba. Baadhi ya maafisa walioathiriwa, inaeleweka, wamefanya kazi Bungeni kwa miongo kadhaa na wanakaribia kustaafu.
Wengine ni wafanyikazi wa chini ambao waliajiriwa takriban miaka miwili iliyopita. Baadhi ni wasaidizi wa maofisa wakuu katika uongozi wa Bunge wakiwemo wanaofanya kazi kwa baadhi ya makamishna.
"Ni mbaya. Tunapozungumza leo, zaidi ya watu 200 wamerudishwa nyumbani. Hatujui kitakachotokea [kwao] lakini hawapo hapa," chanzo kinachofahamu uchunguzi huo katika Bunge kilisema.
Jaribio la The Star kupata maoni kutoka kwa mwenyekiti wa PSC Moses Wetang’ula, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Kitaifa, hazikufua dafu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!