Wikendi iliyopita, staa wa dancehall kutoka Jamaica Garfield Delano Spence almaarufu Konshens alikuwa nchini Uingereza ambapo alifanya tamasha katika jiji la London.
Tamasha hilo la kusisimua lilihudhuriwa na watu wa tabaka mbalimbali, wakiwemo Wakenya kadhaa wanaoishi Uingereza waliokwenda kufurahia muziki wake.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria shoo hiyo walionekana wakipeperusha bendera ya Kenya wakati Konshens akitumbuiza, jambo ambalo lilimshangaza sana mwimbaji huyo wa Jamaica.
"Ikiwa nitafanya shoo mwezini, kutakuwa na Wakenya waliovaa suti za anga naahidi," Konshens alisema, huku akizungumzia uwepo wa Wakenya katika shoo yake ya London.
Sio mara ya kwanza kwa nyota huyo wa dancehall kwenda kutumbuiza katika nchi ya kigeni na kushuhudia baadhi ya mashabiki wa Kenya wakihudhuria.
Katika miaka kadhaa iliyopita, mwimbaji huyo ameonyesha wazi upendo wake kwa Kenya na Wakenya kwa upande wao pia wameendelea kuonesha upendo na sapoti yao kubwa kwake kiasi cha kumpa hata jina la Kikenya na kumtengenezea kitambulisho cha Mkenya.
Wakati akitumbuiza nchini Ujerumani mwezi Julai mwaka huu, Konshens aliiona bendera ya Kenya ikiwa imeshikwa na mmoja wa shabiki aliyehudhuria tamasha na tukio hili likamguza roho kiasi cha kuomba bendera hiyo ili kuonyesha kusimama kwake na taifa la Kenya.
Alipokuwa kwenye pilkapilka ya uimbaji, Konshens aliangalia mbele ya umati na kumtambua shabiki aliyeshikilia bendera ya Kenya akiwa kwenye mstari wa mbele kabisa kwenye tamasha hilo.
Aliuliza umati kama kuna mtu yeyote kutoka Kenya kisha akashirikiana nao kwa furaha na bashasha.
Alichukua bendera hiyo na kuionyesha wakati alipokuwa akiimba, na hata kuomba mashabiki waiinamishe mbele na kuipeperusha jukwaani. Baadaye, aliirudisha kwa mshabiki aliyekuwa ameishikilia.
Aidha, Konshens aliwashirikisha wanawake wakati wa tamasha hilo, akisisitiza kuhusu umuhimu wa wanawake huru na kujitambulisha kama msanii kutoka Kingston, Jamaica.
Vilevile aliitambua pia Uganda wakati wa burudani yake kwenye tamasha hilo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!