
Mchekeshaji na mtangazaji wa redio wa humu nchini Dr Ofweneke amevunja kimya chake baada ya kufananishwa na mwanamume anayevuma kwenye mitandao ya kijamii kutoka nchini Equitorial Guinea.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ofweneke alichapisha picha mbili, yake na ya huyo mwanamume zikiwa zimeunganishwa pamoja na kudai kwamba amekuwa akizipokea kama hizo nyingi kwenye DM zake.
Ofweneke alisema kuwa ametumiwa picha hiyo ikiwa imeunganisha nyuso mbili kama njia ya kufananisha, na kukanusha madai kwamba anafanana na mwanamume huyo.
Kwa mujibu wa Ofweneke, yeye na mwanamume huyo kutoka Equitorial Guinea hawafanani hata kidogo hivyo watu wanastahili kukoma kumtumia picha hiyo ya ufananisho
. “Guys mimi na huyu jamaa hatufanani, muache kunitumia,” alisema na kuambatanisha ujumbe wake na emoji za kulia.
Mwanamume husika kutoka Equitorial Guinea amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii tangia Jumatatu baada ya kudaiwa kuwa alirekodi video za wanawake zaidi ya 400 akishiriki mapenzi nao.
Video hizo zimevujishwa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wanawake mbalimbali, japo haijabainika kama idadi hiyo ya 400 ni kweli ama chagizo.
Taarifa zinadai kwamba serikali ya taifa hilo la Afrika Magharibi imechukua hatua ya kisheria si tu kwa mwanamume huyo ambaye alikuwa ni mfanyikazi wa serikali lakini pia wanawake hao.
Ilidaiwa kwamba wengi wa wanawake kwenye video zake ni wafanyikazi katika serikali na wengine ni watu wa ukoo na wafanyikazi wa serikali.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!