
Malkia wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya na ukanda wa Afrika Mashariki, Nadia Mukami amefichua kwamba wikendi iliyopita, alijipata katika tukio baya la kutishia afya yake akiwa ukumbini.
Mukami, ambaye kwa sasa anatamba na albamu yake ya ‘Queen of the East’ alikuwa akitumbuiza kwenye hafla moja ambapo amefichua kuwa kulitokea hjitilafu ya afya yake wakati anamalizia kutumbuiza akielekea nyuma ya ukumbi.
Mama huyo wa mtoto mmoja alisema alizimia baada ya kumaliza kutumbuiza na hangeweza kutembea kuelekea nyuma ya ukumbi kutokana na kifua chake kumuuma kutokana na kile alichokiita kuwa huenda ni ugonjwa wa pumu.
“Jana Wakati wa #OktobaFest nilikuwa na nguvu za aina yake na vibes kwenye jukwaa hadi kifua changu kikashindwa kustahimili tena na nikapata shambulio la pumu na Kuanguka nilipokuwa nikirudi nyuma ya jukwaa!” Mukami alisema.
Kutokana na hali hiyo, mshindi huyo wa tuzo ya AFRIMMA kitengo cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki mwaka jana ametangaza kuchukua likizo ya muda kutoka kwa shughuli zozote za muziki.
Alisema kwamba imembidi kuchukua hatua hiyo ili kuzingatia afya yake, na kuwa atarejea kwenye ukumbi kutumbuiza kuanzia tarehe 15 daktari wake atakapompa hakikisho kuwa afya yake ik imara kustahimili vishindo vya kutumbuiza kwenye steji.
“Nimekuwa mgonjwa kwa muda na baada ya wikendi hii nitapumzika hadi tarehe 15 ili kutunza afya yangu! Asante sana kwa Dancers, DJ na timu yangu kwa jibu la haraka! Kwa timu ya #OktobaFest asante kwa wema wako. Mla nyama katika wachache, Maua tuonane Usiku wa Leo!!” alisema.
Hii si mara ya kwanza kwa waqsanii nchini Kenya kuanguka wakiwa kwenye steji. Mapema mwaka huu.
Tukio kama hilo lilimtokea msanii Stevo Simple Boy ambaye alianguka na kuzirai akiwa anatumbuiza kwenye kipindi cha 10Over10 kwenye runinga ya Citizen.
Miezi michache iliyopita, msanii Prezzo pia alianguka akiwa jukwaani na wiki kadhaa baadae, akatangaza kubadili muziki wake na kuanza kuimba injili baada ya kupata wokovu katika kanisa la ECC linaloongozwa na Lucy Natasha.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!