Aliyekuwa msanii wa injili, Weezdom hatimaye amezungumzia tatizo lake la afya ambalo limemfanya kuzuiliwa hospitaqlini kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.

Akizungumza katika mazungumza na kituo kimoja cha redio humu nchini, Weezdom aliwashukuru baadhi ya wasanii ambao walijitokeza kumpa msaada lakini pia akashangaa mbona wasanii wengine walikaa kimya muda wote.

Msanii huyo amekuwa akilia kupitia ukurasa wake wa Instagram akiomba wahisani kumsaidia kulipa gharama ya matibabu baada ya kuzuiliwa licha ya kupona mapema.

Akifichua kuhusu tatizo lililompelekea kulazwa, Weezdom alisema;

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Mimi nilikuwa mgonjwa nikalazwa na kisha baadae nikatumwa katika hospitali nyingine huko Limuru. Ni mwili tu ulikuwa na tatizo ila namshukuru Mungu niliweka kutibiwa lakini bado sijatoka kwa sababu sikuwa nimemaliza kulipa bili yote,’ alisaema.

Alikanusha kwamba alikuwa ameenda katika kituo cha kurekebisha tabia kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

“Shida yenye nimekuwa nayo ni kuhusu viungo vyangu vya mwili, na pia nilikuwa na depression iliyoniletea ulcers na pia nikapatikana na condition nyingine inaitwa ADHD, hivyo nilihitaji mahali ambapo ningeweza kupata matibabu ya kimwili na kisaikolojia pia,’ alisema.

Msanii huyo aliwashukuru baadhi ya wasanii wa karibu naye ambao walimsaidia akisema kuwa halikuwa lengo lake kuomba msaada nje ya marafiki zake lakini bili ilivyokwea zaidi, ilimbidi arudi kwenye mitandao kuomba msaada kwa mashabiki.

“Nililazwa Julai 24 na mpaka leo niko hospitalini na natumaini nitaweza kumaliza na nitoke. Bili ilikuwa juu sana lakini tumejaribu kuikata. Marafiki zangu ambao wamekuwa name katika safari hii ambayo haijakuwa rahisi mheshimiwa Jaguar, Guardian Angel, Willy M Tuva, tumeng’ang’ana sana, sikutaka ifike mahali ambapo ningekuja kuomba usaidizi nje ya marafiki zangu lakini hao wamenishika mkono.”

Alisema kwamba bili ambayo imebakia ni kidogo kuliko yenye ambayo alikuwa anadaiwa awali.

‘Sasa ile ambayo imebakia sio kubwa sana, sasa hivi nadhani imebakia elfu 47,” msanii huyo aliongeza.