Naibu wa rais mpya Profesa Kithure Kindiki ametoa ahadi ya kipekee kwa rais William Ruto, pindi baada ya kula kiapo kuhudumia taifa chini yake kama naibu wa rais.

Akizungumza kaitka ukumbi wa KICC katika hafla ya kipekee ya kuapishwa kwake, Kindiki alimshukuru Ruto na kumtaja kama mwalimu wake wa kisiasa na kuahidi kwamba hatokuja kumuangusha hata siku moja katika majukumu yake atakayompa.

“Mheshimiwa rais, maneno yamenikosa kujieleza jinsi ninavyo na furaha leo. Niseme kwamba ninamshukuru Mwenyezi Mungu ambaye anaongoza kila hatua na kila kitu cha kila mwanadamu duniani. Nina shukurani kwako rais kwa heshima ambayo umenipa kufanya kazi chini yako,” Kindiki alisema.

“Mheshimiwa rais, mimi nimekuwa mwanafunzi wako wa kisiasa kwa karibia miaka 20 sasa, na hakuna kitu katika ulingo wa kisiasa ambacho kimenisaidia kujifunza zaidi ya muda ambao nimetembea na kufanya kazi karibu na wewe katika nafasi tofauti. Kwa hivyo mheshimiwa rais ninashukuru. Hivyo nakuahidi mbele ya huu umati na mbele ya Mungu kwamba sitakuangusha kwa upendeleo ambao umenipa leo,” Kindiki aliongeza.

Anamrithi aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ambaye alitimuliwa. Kabla ya kuteuliwa na Rais William Ruto, Kindiki aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa.

Baadaye alithibitishwa na Bunge. Kiti cha majaji watatu katika Mahakama ya Juu kiliondoa amri zilizokuwa zimezuia kiapo cha Kindiki siku ya Alhamisi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kindiki alifika katika ukumbi wa kuapishwa, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC)