Rais William Ruto ametoa ahadi ya kila mtoto kupokea chakula cha afya na chenye lishe bora shuleni ifikapo mwaka wa 2030.

Akizungumza wakati bwa mkutano kuhusu chakula shuleni, rais Ruto alisema mpango wa kutoa chakula shuelni uliopo kwa sasa unawanufaisha zaidi ya watoto milioni 2.6.

“Awali mpango huu ulikuwa unatekelezwa Nairobi pekee, hata hivyo, ujio wa shirika la chakula duniani kulibadilisha vitu na kupanua mpango huo kote nchini.

Matokeo yake yamekuwa ya kutia moyo sana na si siri kwamba Kenya ilirekodi takwimu kubwa za watoto kuenda na kusalia shuleni,” rais Ruto alisema.

Serikali sasa inasalia kuwafikia watoto shuleni na chakula hicho wapatano milioni 10 ifikapo mwaka wa 2030. Mkuu wa taifa hata hivyo alijutia kwamba licha ya mpango huo, tatizo la njaa bado linasalia kuwa sugu kwa watoto wengi.

‘Bado tuna watoto wengi wasioenda shuleni na ndio sababu mimi binafsi nilimuuliza gavana wa Nairobi kwamba hatuwezi kuwa na jiji kuu la Kenya lenye watoto wengi nje ya shule kwa sababu ya vitu viwili; miundombinu shuleni na njaa,” Ruto alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kutokana na hali hiyo, Ruto alifichua lengo la serikali kuhusu mpango wa kulisha shuleni. "Ili kukabiliana na hili, tumeongeza mara tatu mgao wa bajeti ya kulisha shuleni na kuweka lengo bayana: kupanua wigo wa programu kutoka milioni 2.6 hadi watoto milioni 10 ifikapo 2030," alisema.

Rais alizungumza Jumanne wakati wa mkutano wa pili wa mawaziri wa muungano wa kimataifa wa chakula shuleni.

Kufikia wakati huu, Ruto alisema serikali ilizindua mpango wa utendakazi wa kuongeza mpango huo mapema mwezi huu.

"Tumejitolea kuchukua hatua na tumedhamiria kikamilifu kufanikiwa," alisema. Alibainisha kuwa kufikia mwaka wa 2018, mpango huo ulikuwa umeunganishwa kikamilifu kama mpango wa kitaifa, sasa unanufaisha wanafunzi milioni 2.6 - ongezeko la zaidi ya mara kumi kutoka 240,000 la awali.