Mkali wa rap kutoka humu nchini, Khaligraph Jones amedokeza ujio wa kolabo yake ya nguvu na msanii wa ngoma za Agikuyu – Mugithi, Samidoh.

Kupitia Instagram yake, Khaligraph Jones alichapisha picha yake wakiwa na Samidoh na kuiambatanisha na kidokezo hicho.

Alifichua kwamba mipango yote kama itaenda sawa, basi mashabiki wao watarajie ngoma kabla ya kukamilika kwa mwaka huu, ikiwa imesalia miezi miwili tu kuuaga 2024.

“Kabla mwaka uishe Tunawapikia mugithii na @samidoh_muchoki , mtanijua nyinyi #respecttheogs,” Khaligraph Jones aliandika.

Ikiwa watafanikisha ngoma hiyo, Samidoh atakuwa amefanya kolabo ainati nje ya muziki asili wa Mugithi, kwani hapo awali ameshirikiana na wasanii mbalimbali kuachia ngoma zenye ladha mpya.

Mwaka jana, waliachia ngoma na mkali wa Ohangla, Prince Indha, ambayo ilileta ladha ya Rhumba ya kisasa kwa kuchanganya ohangla na Mugithi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wengi sasa wanasubiria kuona kolabo yake na Khaligraph Jones itakuwa nacladha gani, ikizingatiwa kwamba msanii huyo ni wa hiphop na yeye ni wa Mugithi.