
Wawili hao walikuwa wanatumbuiza katika mwendelezo wa tamasha la Wasafi Festival maeneo ya Muleba ambapo walipiga shoo ya kikoa jukwaani, shukrani kwa kolabo yao ya nguvu ‘Mtasubiri sana’.
Wakiwa jukwaani, Diamond aliibua utani wake kama kawaida akitaka kujua ikiwa kweli Zuchu anampenda au ako naye kwa sababu ya umaarufu na utajiri wake tu.
Msanii huyo ambaye tayari ana watoto na warembo zaidi ya wawili alisikika akimsihi Zuchu kama kweli anampenda basi afanye kumzalia, jambo ambalo Zuchu japo alitabasamu lakini alionyesha ishara ya kulikataa kwa kidole.
Zuchu naye alimkaba Diamond kwa swali lilo hilo akilenga kujua iwapo bosi wake anampenda kweli ana analenga kumchezea na kisha baadae kumuacha kama alivyofanya kwa warembo wengine aliozaa nao.
Zuchu alimkumbusha Diamond kama kweli anampenda na anataka kuwa na mtoto naye, basi afanye kumuoa rasmi kwa harusi kwanza ili awe huru kubeba ujauzito wake.
“Je unaniamini? Utanizalia?” Diamond alimuuliza huku Zuchu akiunga mkono kwa ishara ya kukataa.
“Nauliza unanipenda mimi na unanitaka? Utanioa lini ndio nikuzalie?” Zuchu alimtupia Diamond jibu kwa njia ya swali na kumuacha mdomo wazi, huku akimuonyesha kidole chake bila pete.
Wawili hao wamekuwa wakionyesha kila dalili na ishara ya kupendana tangu mapema mwaka 2022 walipodai kwamba kungetokea na jambo lao kuu la kuoana wakati wa siku ya wapendanao, Februari 14.
Hata hivyo, mendelezo wa vitimbi vyao vya mapenzi umekuwa ukishuhudiwa kiasi kwamba baadhi ya mashabiki wao wameshawishika wawili hao si wapenzi bali wamejificha kwenye kiza cha mapenzi ili kuendeleza ajenda ya kuuza kazi zao za Sanaa.
Je, wewe unaamini wawili hawa ni wapenzi ama ni kiki tu?
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!