Chama cha ODM kimepinga vikali mswada unaolenga kuongezwa kwa muda wa muhula wa kisiasa nchini.

Katika taarifa, chama hicho kiliwarai maseneta wake kupiga kura ya kupinga kupitishwa kwa mswada huo unaotaka kuongezwa kwa muda wa muhula wa kisiasa kutoka miaka 5 hadi 7.

Mswada huo umewasilishwa na seneta wa Nandi, Samson Cherargei.

"Kwa hivyo tunaitaka Seneti kukataa Mswada huu na kuzingatia kanuni za utawala bora, utawala wa sheria na matakwa ya kikatiba ya ushiriki wa umma wa kweli kupitia kura ya maoni ya umma," Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha ODM Odor Ong’wen alisema.

Ong’wen alithibitisha kuwa marekebisho yanayopendekezwa yanakiuka vifungu kadhaa vya katiba ikiwa ni pamoja na sheria zinazohusiana na ukuu wa Katiba, Mswada wa Haki na uhuru wa watu.

“Tunataka kusajili wasiwasi wetu kwa kueleza kukataa kwetu kabisa Katiba inayopendekezwa ya Kenya (Marekebisho) Na. 2, 2024 kwa ujumla wake. Kukataliwa huku kunatokana na ukiukaji wa kifungu cha 255 (1) cha Katiba ya Kenya, 2010 na kubatilisha muundo wake wa kimsingi,” aliongeza..

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mswada wa Seneta wa Nandi Samson Cherargei unalenga kuongeza muda wa kukaa ofisini kwa rais, magavana na Wabunge kutoka miaka mitano hadi saba, miongoni mwa marekebisho mengine ya katiba