
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi nchini humo, mwanamke huyo kwa jina Josephine Nyapendi alidai kwamba aliletewa maono ndotoni na roho mtakatifu kuhusu bunduki hiyo haramu nyumbani kwa jamaa kwa jina Vincent Emodo.
Na kweli kwa maneno yake, baada ya kuwaongoza polisi hadi katika nyumba ya Emodo ambapo bunduki hiyo ilipatikana chini ya kitanda na kupelekea kukamatwa kwake.
“Taarifa hizo zilitolewa na Nyapendi Josephine ambaye alidai kuwa aliingiwa na roho mtakatifu hivyo kumfanya afichue uwepo wa bunduki hiyo kwa Onyapidi Alfonse aliyekuwa akiendesha maombi wakati huo,” msemaji wa polisi alisema.
Msemaji huyo wa polisi, alitaja kuwa katika upekuzi huo, polisi waligundua bunduki aina ya SMG ikiwa na risasi tayari.
"Upekuzi zaidi katika nyumba ya Emodo Vincent ulifichua jarida moja lililokuwa na risasi 29," aliongeza.
Kulingana na msemaji wa polisi, Emodo alikuwa ametoroka ili kukwepa kukamatwa wakati silaha hiyo ilipopatikana.
Walakini, polisi walifanikiwa kumkamata mnamo Oktoba 27, 2024.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!