Mtayarishaji wa maudhui mashuhuri Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy ameweka wazi kwamba alipata jeraha dogo tu baada ya kuhusika katika ajali wikendi.

Video zinazoonyesha tukio la ajali zilivuma kwenye mitandao ya kijamii zikiibua wasiwasi kuhusu hali ya mtayarishaji maudhui huyo mwenye umri wa miaka 22.

Siku ya Jumapili, alishiriki video zinazoonyesha jeraha dogo ambalo alipata katika tukio hilo la kutisha ambalo liliona gari alilokuwa akiliendesha likitua kwenye mtaro. “Ukitazama paji la uso wangu utaona mchubuko,” Pritty Vishy alisema.

Aliongeza, “Broo, ata sijui nilijigonga wapi, lakini weeeh.” Katika video nyingine, alionekana akionyesha mchubuko ulio upande wa kulia wa paji la uso wake.

"Penye niliumia wakati wa ajali.. sijui niligonga wapi lakini heeh,"

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baada ya kuhusika katika ajali hiyo siku chache zilizopita, Vishy alienda kwenye Instastory yake kumpa taarifa kuhusu hali yake baada ya Wakenya kuhoji ikiwa yuko sawa.

 

"Jeraha dogo tu, lakini niko vizuri," alisema.