Msanii mkongwe wa miziki ya sekula, Jackson Ngechu maarufu kama Prezzo ametangaza kuachana na miziki ya kidunia na kuanza kuimba injili.

Prezzo, anayefahamika kwa kuwa mtunzi na mtumbuizaji wa miziki ya kidunia tangu mapema miaka ya 2000s alitangaza kukutana na wokovu wikendi iliyopita katika ibaada maalumu kwenye kanisa la ECC Nairobi.

Kanisa la ECC Nairobi linaongozwa na mchungaji Lucy Natasha.

Msanii huyo alimmiminia sifa mchungaji huyo pindi alipopanda kwenye mimbari na kushika maikrofoni.

Alisema kwamba Natasha amekuwa moja kati ya mihimili mikuu katika safari yake ya kugeukia miziki ya injili na hata kuenda mbele kuwaonjesha waumini sehemu ya kibao chake kipya cha injili.

“Ningependa kutoa shukrani za kweli kwa mchungaji wangu Natasha. Unajua kama si wewe mimi nisingekuwa katika eneo hili la injili. Unaelewa, na mimi ninataka kufanya wimbo kwa Mungu,’ Prezzo alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

‘Na ninahisi kuwa mbarikiwa wakati huu ninapoenda kuonjesha wimbo,” aliongeza huku akianza kuimba kwa shangilio.

Kwa upande wakwe, mchungaji Natasha alimhongera Prezzo kwa kutoa maisha yake kwa kumtumikia Mungu, baada ya kuwaburudisha mashabiki kwa nyimbo za kidunia kwa karibia miongo miwili.

“Unapoingia Uweponi Kwake Kwa Sifa Anaingia Katika Mazingira Yako Kwa Nguvu! ? Hongera sana Mwanangu wa Kiroho @prezzo254 kwa kuachia wimbo wako mpya wa Injili uliozinduliwa leo @eccnairobi. Mungu akutumie kuwafikia vijana wetu. Kizazi chetu ni Wajibu Wetu. Najivunia Wewe Mwana,” Rev Lucy Natasha alionyesha fahari yake kwa Prezzo.

Mashabiki wengi kwenye ukurasa huo wa Instagram walimpokea Prezzo kwa mbwembwe wakimtaka kuendeleza injili kwa nguvu na ari sawia na alivyofanya katika kupakua burudani ya sekula.

@officialfrankrobinson: “Ndugu yangu @prezzo254 karibu katika ufalme wa Mungu?”

@princessirene792: “Endelea kupaa juu zaidi..??hii ndio njia bora zaidi,hautajuta kumtumikia Mungu.’

@apostle_jacob_major_son_of_the_oracle: “tunakupenda mr prezo at Ecc, keep shinning under Neema ya mama yetu wa kiroho.”

@christine_zawadi: “Nilibarikiwa sana kukuona kanisani, Wewe ni mteule wa Mungu.”

@jawamu.lifestyle: “Karibu kwenye Kingdom prezzo Wanaume Halisi wanampenda Yes