Muigizaji wa zamani wa kipindi cha Tahidi High, Gloria Moraa maarufu kama Actress Nyaboke anaomboleza kifo cha babake.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Nyaboke alichapisha picha ya marehemu bintiye na baba yake akiwa ameketi na kufichua kwamba mzee huyo amekata pumzi usiku wa kuamkia leo.

Nyaboke aliomboleza mzee baba akisema kuwa alikuwa nguzo muhimu katika kumfariji wakati alipompoteza bintiye miezi mitatu iliyopita.

“Mnamo tarehe 28 Julai binti yangu alipumzika, imekuwa ngumu. Siku hiyo hiyo miezi 3 baadaye mwamba wangu imara, babu yake ameamua kutoamka,” Nyaboke aliomboleza.

“Mwanaume huyu ambaye nampenda hadi kufa, alinipenda bila masharti. Maneno yake ya mwisho kwangu "Nyargot mwanangu, nakupenda na Mungu anakupenda sana, tulia wewe mama" Ei nina maumivu sana, kiasi nahisi kama ninaipoteza. Rest in peace baba. Huu mwaka nao umeamua kunivunja ntapimzikia mbinguni.eii,” aliongeza.

Mnamo JULAI 28, Nyaboke alipata pigo kuu baada ya kufiwa na mzawa wake wa kwanza Marrie ambaye alikufa katika mazingira tatanishi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mashabiki wake kupitia Instagram walimfariji kwa jumbe mbalimbali za kutia moyo;

@laurene_ash23: “Aki 2024 imekuwa mbaya sana kwako mamaa?alot of hugs ??? dear ,Mungu akufariji katika kipindi hiki kigumu ?”

@_yolobabes: “Hugs mama siku bora mbele.”

@brenda_kiarie: “Neema na nguvu zaidi kwa familia yako!!” @achitsal: “Sio tena Bwana hii ni kubwa kwa mtu mmoja ??? pole moraa.”