
Kupitia Instagram, Simple Boy alichapisha video akiwafokea wasanii Willy Paul na Bahati na kuwatabiria kwamba hatima yao ni jehanamu moja kwa moja.
Alianza na Willy Paul akimsuta kwa wimbo wake wa ‘Mbinguni hakuna digrii’ na kutaka kujua Pozee alijuaje kwam ba mbinguni hakuna digrii hali ya kuwa hajawahi fika kule.
Alisema kuwa huo ni uongo na kutokana na kudanganya kwake, moja kwa moja atatua jehanamu.
“Willy Paul ulisema mbinguni hakuna digrii, wewe ulienda mbinguni ukapata hakuna digrii? Wacha uongo. Wewe unaenda jehanamu,” Stevo Simple Boy alisema.
Stevo pia hakumsaza Bahati Kioko, msanii waliyehama kutoka injili kwenda katika mizki ya kidunia na Willy Paul.
Alimsuta kwa kuwa mtu wa kujigamba sana katika miaka ya hivi majuzi kinyume na alivyokuwa mnyenyekevu miaka ya nyuma.
“Bahati, ulikuwa mtoto wa baba, sasa hivi umekuwa mtoto wa mama. Na kitambo ulikuwa unalia lia. Siku hivi umekuwa mjeuri,” Stevo aliongeza.
Willy Paul na Bahati wamekuwa wakipokea kusutwa kwa wingi kutokana na kuhama kutoka kwa muziki uliowatambulisha kwenye uwanja wa burudani Kenya.
Wawili hao wamejijengea majina katika Sanaa ya miziki ya kidunia baada ya kugura injili takribani miaka 7 iliyopita.
Hata hivyo, kila mmoja katika maelezo yao wamekuwa wakikanusha kuhama injili wakisisitiza kwamba bado wao ni wachamumungu kindakindaki.
Pozee katika mahojiano ya awali alisisitiza kwamba nusra ajitoe uhai katika kile kilichokuwa kikizunguka maisha yake kwenye injili, akisisitiza kwamba wasanii katika tasnia ya injili hawapendani kama ambavyo inaonekana kwa jicho la nje.
Msanii huyo alisisitiza kwamba japo aliacha kutunga mashairi ya injili, bado yeye ni mchamungu sana, akiutaja uhusiano wake na Mungu kuwa wa kipekee.
Alifichua kwamba hata anapoenda kutumbuiza katika majukwaa mbalimbali, huwa anaomba kabla ya kuanza kutumbuiza, jambo linaloonyesha uhusiano wake na Mungu bado ungali imara.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!