YouTuber Nicolas Kioko na mpenziwe Wambo Ashley wamefichua kwamba kulea watoto mapacha si jambo rahisi kama ambavyo wengi wanalichukulia.

Wakizungumza katika mahojiano na Mungai Eve, Kioko na Ashley walifichua kwamba ujio wa wanao mapacha ulisuka upya mtazamo wao kuhusu maisha kwa ujumla.

Kioko alisema kwamba walikuwa wanatumia takribani shilingi elfu 58 kila mwezi kuwanunulia mapacha hao unga wa maziwa.

Ashley alifichua kwamba aliwanyonyesha kwa miezi ya kwanza 3 tu na akaficha mahali akahisi kulemewa na ndiposa wakahamia katika kuwalisha unga wa maziwa.

“Watoto wametupeleka mbio sana, unajua kulea mapacha si kama kulea mtoto mmoja. Mapacha lazima ukuwe sawa kimfuko. Mimi niliwanyonyesha kwa miezi ya kwanza mitatu na nikalemewa, si kwamba nilikosa maziwa lakini sikuwa na hayo maziwa ya kutosha, lakini ningeweza kuwanynyesha. Ilifika miezi 3 nikachoka, ilikuwa tu inachosha, ukiangalia watoto ni 2 sasa tukasema tu wakunywe maziwa ya unga,” Wambo Ashley alisema.

Kwa upande wake, Kioko alifichua hesabu ya kuwalisha chakula hicho ambacho kinanunuliwa kwa bei ghali.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Huo wakati tulikuwa tunanunua Sh1960 moja ambayo inatumika kwa saa 18. Hiyo ni kama elfu 58 kwa mwezi. Ni ghali sana, mtu usizae kama hauko tayari,” Kioko alisisitiza.

Kuhusu jinsi walijikuta wameanza maisha pamoja kama mke na mume, Kioko alifichua kwamba si jambo ambalo walikuwa wamelipangia bali mimba ilikuwa chanzo.

“Mimba ndio ilifanya tuanze kuishi pamoja. Alikuwa amekataa kabisa kuja kuishi na mimi, ilibidi mpaka nikahama kwenda kwa nyumba nyingine ili aje lakini bado alikataa,” Kioko alifichua.

“Baada ya kuhama, tulikosana. Mimi nikambembeleza nikaona hataki name nikaamua kunyamaza sasa. Siku iliyofuata nikapata ananiandikia ujumbe kwamba anakujia nguo zake jioni. Alikujia nguo na hakuwahi rudi, iliisha hivyo sasa na akapata mimba,” Kioko aliongeza.