Mchekeshaji na mwanaharakati maarufu wa Kenya Eric Omondi amesimulia matukio yaliyopelekea kukamatwa kwake katika bustani ya Uhuru siku ya Jumapili, Oktoba 20.

 

Katika chapisho la Jumapili jioni, mwanaharakati huyo alionyesha video yake akiwa amevalia buibui huku akijaribu kuingia katika bustani hiyo kwa gari lake.

 

Eric alieleza kwenye video hiyo kwamba alipokea taarifa kuhusu jaribio lililopangwa la kumuua ikiwa angetokea katika bustani hiyo.

 

"Niko hapa Uhuru Park kwa sababu lazima nijitokeze, hawajui nipo hapa, lakini niko hapa. Tutadeal na wao vile wanadeal na sisi,” Eric alisema kwenye video kabla ya kufanikiwa kuwapita polisi akiwa kwenye gari lake.

 

Mchekeshaji huyo wa zamani wa Churchill Show aliendelea kusimulia jinsi polisi hatimaye walivyofanikiwa kumkamata kwani hakuweza kukimbia vyema akiwa amevalia buibui.

 

Hata hivyo aliachiliwa baadaye na kupata kusimulia kilichotokea.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 

“NIKO HURU!!! Kwa hiyo nilikuwa Uhuru Park Asubuhi nzima lakini nilijificha kwa sababu nilikuwa nimepewa taarifa na kuambiwa niwe makini,” alisema mcheshi huyo.

 

Aliendelea kusimulia, “Mnamo saa sita adhuhuri polisi wakitufukuza nilishikwa juu sikuweza kukimbia kwenye bui bui. Polisi walishtuka na kugundua ni mimi������������. Muhimu ni kwamba tulijitokeza na Kusherehekea mashujaa wetu."

 

Eric Omondi alikuwa ametoa maagizo kwa Wakenya ambao wangehudhuria hafla yake mbadala ya siku ya Mashujaa katika bustani ya Uhuru Park Jumapili, Oktoba 20, 2024.

Hafla hiyo ilikuwa ifanyike kwa heshima ya Wakenya waliopoteza maisha wakati wa maandamano ambayo kwa kiasi kikubwa yaliongozwa na Gen Z kudai uwajibikaji zaidi serikalini.

 

Alitangaza kuwa Wakenya kutoka matabaka mbalimbali walipaswa kuanza kumiminika katika ukumbi huo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hafla hiyo ikitarajiwa kuendeshwa hadi saa tisa alasiri.

 

Washiriki pia walitarajiwa kubeba bendera ya Kenya na mshumaa pamoja na wazazi wa wale waliouawa wakati wa maandamano yanayotarajiwa kuhudhuria.